Lugha Nyingine
Serikali ya Sudan yakanusha uwepo wa pengo la chakula
Serikali ya Sudan imekanusha uwepo wa pengo la chakula nchini humo na kuzitaja ripoti za awali za njaa nchini humo kuwa "zimetiwa chumvi".
Kaimu Waziri wa Kilimo wa Jimbo la Khartoum Mohamed Siral-Khatim jana alisema katika taarifa yake kuwa hakuna pengo la chakula, na hakuna njaa katika jimbo la Khartoum au majimbo mengine, akiongeza kuwa labda kuna uhaba wa usambazaji chakula katika maeneo yanayodhibitiwa na wanamgambo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
Siral-Khatim amesema amekagua baadhi ya miradi ya uzalishaji wa kilimo na wanyama katika sehemu ya kaskazini ya Omdurman, mji ulioko kaskazini mwa mji mkuu wa Sudan Khartoum, na kugundua kuwa miradi hiyo "inazalisha chakula cha kutosha kwa maeneo yote salama" kaskazini mwa Omdurman.
Siral-Khatim pia amesema serikali ya Jimbo la Khartoum inataka kushinda vizuizi vinavyowakabili wakulima, ikifanya kazi ya kuwapatia mafuta, mbegu bora na mbolea.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma