Lugha Nyingine
Faustine Engelbert Ndugulile wa Tanzania achaguliwa kuwa mkurugenzi mpya wa kanda ya Afrika wa WHO
(CRI Online) Agosti 28, 2024
Faustine Engelbert Ndugulile wa Tanzania Jumanne alichaguliwa kuwa mkurugenzi mpya wa kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO), ambaye anachukua nafasi ya Matshidiso Moeti aliyeshika wadhifa huo tangu mwaka 2015.
Mkurugenzi huyu mpya alichaguliwa kwenye mkutano wa 74 wa Kamati ya Kanda ya Afrika ya WHO, kutoka wagombea wengine watatu, wakiwemo Boureima Hama Sambo wa Niger, Richard Mihigo wa Rwanda na Ibrahima Soce Fall wa Senegal. Kiongozi huyo mpya anadhamiria kuendelea kufanya mageuzi, ili kuboresha mazingira ya matibabu na afya ya watu wa Afrika, na kukabiliana na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mpox.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma