Lugha Nyingine
Kenya kuchukua hatua kuboresha viwango vya mikopo
Hazina ya Kitaifa ya Kenya imesema inafanikisha uimarishaji wake wa fedha, kuboresha utendaji wa mauzo ya nje, na kupanua akiba ya kigeni ili kuboresha viwango vyake vya mikopo huru.
Katika ripoti yake hazina imesema kuwa shughuli hizo zitaifanya nchi hiyo kuongeza hatua kwa hatua viwango vya uwekezaji (BBB-) na kuvutia madeni nafuu katika masoko ya kimataifa.
The Standard & Poor's (S&P) Jumamosi ilishusha viwango vya nchi hadi B- kwenye uimarishaji dhaifu wa fedha. Hatua hii ilifuatia Kenya kufutilia mbali mpango wake wa kuongeza mapato kwa 2024/2025, huku S&P ikibainisha kuwa hatua hiyo itashuhudia gharama za kulipa deni ikizidi asilimia 30 ya mapato ya serikali katika kipindi cha 2024-2027.
Rais wa Kenya William Ruto aliondoa mpango wa kukusanya fedha za nyongeza shilingi bilioni 346.7 (kama dola bilioni 2.7 za Kimarekani) ili kufadhili bajeti yake ya dola bilioni 31 kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025.
Kwa mujibu wa ofisi ya kitaifa ya takwimu, Kenya imeongeza mauzo yake ya nje, huku mapato yakipanda kwa asilimia 28 hadi dola bilioni 2.28 katika robo ya kwanza ya mwaka 2024 kutokana na kuongezeka kwa usafirishaji wa bidhaa za chai na za kilimo cha bustani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma