Lugha Nyingine
Mpango wa ujuzi wa kidigitali wazinduliwa nchini Tanzania
Serikali ya Tanzania itaendelea kutoa kipaumbele katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili iweze kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi kama inavyoelekezwa katika Dira ya Taifa ya 2025 na Sera ya Maendeleo ya TEHAMA ya mwaka 2016.
Hayo yamesemwa jumamosi na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa nchini Tanzania, Dk. Doto Biteko jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa mpango wa Ujuzi wa Kidigitali kwa wote (DigiTrack) uliowezeshwa na kampuni ya Huawei ya China na Vodacom Foundation.
Dk. Biteko amesema, serikali itafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba wawekezaji wanakuwa msaada katika kubadilisha hali ya maisha ya watu kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo TEHAMA huku pia wawekezaji hao wakinufaika na uwekezaji wao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma