Lugha Nyingine
Maafisa wa polisi wa ATMIS wanolewa ili kukabiliana na vifaa vya vilipuzi kwenye vituo vya ukaguzi
Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) kimesema maafisa wake 19 wa polisi wamemaliza mafunzo yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kuhusu ukaguzi wa vituo vya ukaguzi wa magari ili kuimarisha usalama wa kikanda.
ATMIS imesema mafunzo hayo ya siku sita yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kushughulikia Masuala ya Mabomu (UNMAS) ambayo yalifanyika katika mkoa wa Hiran katikati mwa Somalia yalilenga pia kukabiliana na tishio la mabomu (IEDs) kwa raia na miundombinu muhimu.
Kwenye taarifa iliyotolewa Jumamosi jioni, kiongozi wa timu ya Maafisa wa Polisi wa ATMIS Moffat Chungu, alisema mafunzo haya yalilitoa utambuzi kwa sababu yalionesha picha halisi ya kile kinachohitajika kwa kama maafisa wa polisi wakati wa kufanya taratibu za ukaguzi wa magari, kwa nadharia na vitendo.
Chungu amesema kuwa mafunzo hayo yaliyofanyika katika mji wa Beledweyne katikati mwa Somalia ni muhimu kwa mapambano dhidi ya ugaidi, ambapo taifa hilo limekuwa likipambana na uasi wa al-Shabab kwa takriban miaka 20.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma