Lugha Nyingine
Africa CDC yatahadharisha juu ya kuongezeka kwa watu wenye mpox, kiwango cha juu cha vifo na uchunguzi mdogo
Mgonjwa mtoto wa mpox akipata matibabu kwenye hospitali ya eneo la Nyiragongo karibu na Goma, Jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Agosti 15, 2024. (Picha na Zanem Nety Zaidi/Xinhua)
Kituo cha Kudhibiti na Kukinga Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kimetoa tahadhari juu ya mzigo mkubwa wa watu wenye mpox, uwezo mdogo wa uchunguzi, na kiwango cha juu cha vifo vinavyotokana na ugonjwa huo, kama baadhi ya changamoto zinazozuia jitihada za kukabiliana na mpox wakati idadi ya wagonjwa ikiongezeka kote Afrika.
Katika taarifa yake kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa mpox barani Afrika iliyotolewa Ijumaa, Mkurugenzi Mkuu wa Afrika CDC Jean Kaseya, alisema changamoto hizo pia zinahusiana na kuenea kwa kasi kwa ugonjwa huo kwa nchi nyingine na majaribio tofauti ya kushughulikia ugonjwa huo huku kukiwa na mahitaji makubwa ya kuboresha juhudi za uratibu.
Takwimu kutoka Afrika CDC zinaonesha kuwa kuanzia mwanzoni mwa 2024 hadi Agosti 23, jumla ya watu 21,466 wanawezekana kuwa na ugonjwa wa mpox, na vifo 591 vimeripotiwa kwenye nchi wanachama 13 wa Umoja wa Afrika (AU), zikiwemo Burundi, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Cote d'Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Gabon, Liberia, Kenya, Nigeria, Rwanda, Afrika Kusini, na Uganda.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma