久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Mahmoud Abbas asema kutambuliwa kwa Palestina iliyo?na umoja ni ufunguo wa amani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 16, 2024

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas akizungumza katika Bunge la Kitaifa la Uturuki mjini Ankara, Uturuki, Agosti 15, 2024. (Mustafa Kaya/Kitini kupitia Xinhua)

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas akizungumza katika Bunge la Kitaifa la Uturuki mjini Ankara, Uturuki, Agosti 15, 2024. (Mustafa Kaya/Kitini kupitia Xinhua)

ANKARA - Bila kutambuliwa kimataifa kwa Palestina iliyo na umoja, hakutakuwa na amani, mshikamano na ustawi katika eneo hilo, amesema Rais wa Palestina Mahmoud Abbas siku ya Alhamisi kwenye ziara yake katika Mji Mkuu wa Uturuki, Ankara.

Baada ya kukutana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan siku ya Jumatano, rais huyo wa Palestina alitoa hotuba katika Bunge la Uturuki kwa mara ya kwanza tangu mgogoro wa Gaza kuzuka Oktoba mwaka jana.

Kwenye hotuba yake, amebainisha kuwa jumuiya ya kimataifa haipaswi kukaa kimya kuhusu mgogoro huo wa Gaza. Amedokeza kuwa Marekani imetumia kura yake ya turufu mara tatu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzuia maazimio yanayohusu Gaza, na kwamba maazimio yaliyopitishwa kuhusu suala la Palestina hayajatekelezwa.

Rais huyo wa Palestina amesema kutambuliwa kwa taifa la Palestina ndiyo ufunguo wa amani, mshikamano na ustawi wa eneo hilo. Isipokuwa pale tu watu wa Palestina watapata umoja wa kitaifa, itakuwa vigumu kupata ushindi wa mwisho, ameongeza.

Kwa sasa taifa la Palestina linatambuliwa na nchi 145 wanachama wa Umoja wa Mataifa lakini bado ni nchi mwangalizi wa UN, badala ya kuwa nchi mwanachama.

Katika hotuba yake, rais huyo wa Palestina ametangaza kwamba atakwenda Gaza, akisema maisha yake hayana thamani zaidi kuliko watoto wa huko.

Ziara hiyo ya Abbas mjini Ankara imekuja huku idadi ya Wapalestina waliouawa kwenye ukanda wa Gaza kutokana na mashambulizi yanayoendelea ya Israel ikizidi 40,000. Pia kuna wasiwasi unaozidi kuongezeka juu ya uwezekano wa kuenea kwa vita katika kanda hiyo kufuatia mauaji ya kiongozi wa zamani wa Hamas, Ismail Haniyeh nchini Iran.

Serikali ya Iran imeapa mara kwa mara kwamba italipiza kisasi dhidi ya Israel ambayo inaituhumu kutekeleza mauaji hayo.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas akizungumza katika Bunge la Kitaifa la Uturuki mjini Ankara, Uturuki, Agosti 15, 2024. (Mustafa Kaya/Kitini kupitia Xinhua)

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas akizungumza katika Bunge la Kitaifa la Uturuki mjini Ankara, Uturuki, Agosti 15, 2024. (Mustafa Kaya/Kitini kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>