Lugha Nyingine
Rais?Xi asema China ingependa kushirikiana ?na Brazil kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya China na Brazil yenye mustakabali wa pamoja
BEIJING - China ingependa kufanya juhudi pamoja na Brazil na kuchukua maadhimisho ya miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia kama mwanzo mpya kwa kuhimiza kwa pamoja ujenzi wa jumuiya ya China na Brazil yenye mustakabali wa pamoja, Rais wa China Xi Jinping amesema siku ya Alhamisi kwenye salamu zake za pongezi kwa Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil katika siku ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
China na Brazil, zote zikiwa ni nchi kubwa zinazoendelea na zenye masoko muhimu yanayoibukia, ni marafiki wazuri wenye nia moja na washirika wanaoshikana mikono na kusonga mbele pamoja, Rais Xi amesema.
Katika miaka 50 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, bila kujali mabadiliko katika mazingira ya kimataifa, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umedumisha maendeleo thabiti, huku kukiwa na ushawishi unaongezeka duniani ambao ni mkubwa zaidi, wa pande zote na wa kimkakati, na katika wakati wa kuhimiza maendeleo na ustawishaji wa mataifa yao, China na Brazil pia zimetoa mchango mkubwa kwa ajili ya amani, utulivu na ustawi wa dunia, Xi amesema.
China ingependa kuchukua maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia na Brazil kama mwanzo mpya kwa kuimarisha kuoana kwa mikakati ya maendeleo kati ya nchi hizo mbili kila wakati, kuzidisha mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali, kuongeza ukurasa mpya wa zama tulizonazo kwenye uhusiano kati ya China na Brazil, na kufanya juhudi za pamoja za kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya China na Brazil yenye mustakabali wa pamoja, amesema.
Rais Lula amesema katika salamu zake za pongezi kuwa, katika miaka 50 iliyopita, urafiki kati ya Brazil na China umeimarishwa, na ushirikiano umezidi kuwa wa aina mbalimbali.
Ameongeza kuwa, kwa sasa, nchi hizo mbili zinadumisha ushirikiano katika sekta nyingi na kwenye ngazi zote, ili kwa pamoja kujenga dunia yenye ustawi, amani na haki.
Amesema kwa miaka 50 ijayo ya uhusiano wa nchi hizo mbili, nchi hizo mbili zitashirikiana bega kwa bega kwa kuanzisha njia mpya na kujenga mustakabali mzuri wa pamoja wa siku za baadaye.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma