久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Mapinduzi ya harusi za kufurahia “kidogo ni zaidi” nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 14, 2024

Wanandoa wapya wakifanya karamu ya harusi kwenye basi katika Eneo la Fuling, Mji wa Chongqing, Kusini Magharibi mwa China, Mei 12, 2024. (Xinhua)

Wanandoa wapya wakifanya karamu ya harusi kwenye basi katika Eneo la Fuling, Mji wa Chongqing, Kusini Magharibi mwa China, Mei 12, 2024. (Xinhua)

Kwakuwa Xiao Peng mwenye umri wa miaka 26 alikutana na mpenzi wake wa kiume kwenye basi katika Eneo la Fuling la Mji wa Chongqing, Kusini Magharibi mwa China, wapenzi hao kwa silika walijua ni gari gani litakuwa sahihi kwa harusi yao. Walichagua basi kuwa gari la harusi yao.

“Ikilinganishwa na msafara wa magari ya harusi ya kijadi, mabasi ni rafiki kwa mazingira ya asili, na ya bei nafuu zaidi,” amesema, akiongeza kuwa karamu ya harusi yake ilitumia safari hiyo ya basi kuimba nyimbo, kupiga picha na kukumbushana mambo mbalimbali.

Hata hivyo, harusi kama hizo za kipekee siyo za kawaida sana nchini China, ambako harusi za kijadi huwa zenye ufahari mwingi pamoja na misafara mirefu ya magari, desturi nyingi na orodha ndefu ya wageni waalikwa.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Guyu Data, jukwaa la uchambuzi wa takwimu na maoni ya jamii chini ya kampuni ya Tencent News, mnamo 2021, wastani wa gharama za matumizi ya harusi kwa vijana wa China ulikuwa Yuan karibia 174,000 (takriban dola 24,530 za kimarekani), ambao ni mara 8.8 ya wastani wa kipato cha kila mwezi cha kila wanandoa. Asilimia 42 kati ya wanandoa waliohojiwa kwenye utafiti huo walikiri kuwa harusi zao zilipita bajeti zao za awali.

Kama ilivyo kwa Xiao Peng, siku hizi vijana wengi zaidi wa China wanaachana na taratibu nyingi za harusi za kijadi. Wanaamini kuwa kupitia kujikita kwa kiasi kidogo kwenye desturi na taratibu, wanaweza kujikita zaidi katika mambo ya kukumbushana, hisia na maana halisi ya ndoa.

Lin Mo mwenye umri wa miaka 34 anayeishi Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China alifanya harusi yake rahisi mwaka huu. “Mume wangu na mimi tuliandaa harusi wenyewe, na hafla kuu ilidumu kwa dakika 10 tu, ambapo katika muda huo tulihutubia wageni kwa ufupi na kuvalishana pete,” ameeleza.

Lin anaamini kuwa upendeleo wa harusi za kifahari miongoni mwa Wachina wengi unatokana na umuhimu wanaoweka katika “mianzi”, neno linalomaanisha heshima au hadhi ya mtu katika lugha ya Kichina.

“Nadhani harusi ni mambo binafsi, siyo ya kuonesha kwa wengi. Kwa hivyo tulijikita zaidi kwenye kukumbushana mambo yetu na kubakisha mambo ambayo tunaamini ni muhimu zaidi na kutupatia thamani ya kutosha ya kihisia,” amesema Lin.

“Harusi za kijadi nchini China zinahusisha mfululizo mgumu wa sherehe ambazo zimekita mizizi katika historia, na huenda haziendani na kasi ya maisha ya hivi leo. Harusi za kurahisishwa na za binafsi ni chaguo lenye mantiki kwa wanandoa vijana, kwa kuwa zinasaidia kupunguza shinikizo la kifedha na kuongeza furaha zao,” amesema Mei Zhigang, naibu profesa wa Shule ya Sosholojia ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Katikati ya China.

Harusi ya pamoja ya wanandoa wengi ikifanyika katika Eneo la Xinzhou, Mji wa Wuhan, Mkoa wa Hubei, Katikati ya China, Mei 18, 2024. (Xinhua)

Harusi ya pamoja ya wanandoa wengi ikifanyika katika Eneo la Xinzhou, Mji wa Wuhan, Mkoa wa Hubei, Katikati ya China, Mei 18, 2024. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>