Lugha Nyingine
China yaeleza?wasiwasi juu ya idadi kubwa ya vifo vya raia vilivyosababishwa na operesheni za kijeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian amesema, China ina wasiwasi mkubwa juu ya idadi kubwa ya raia waliouawa kutokana na operesheni za kijeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza.
Li Jin amesema hayo alipozungumzia shambulizi la Jeshi la anga la Israel dhidi ya shule moja katika Ukanda wa Gaza lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita siku ya Jumamosi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 100.
Bw. Lin amesema China inalaani kitendo chochote kinachoathiri raia, inapinga ukiukaji wowote wa sheria za kimataifa za kibinadamu, na kuitaka Israel kusikiliza kwa makini wito wa jumuiya ya kimataifa, kusitisha mara moja mapigano na kulinda raia kwa nguvu zote, ili kuzuia hali ya wasiwasi katika kanda hiyo isizidi kuongezeke.
Pia amesisitiza kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya juhudi za pamoja ili kupunguza na kumaliza janga la kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma