Lugha Nyingine
Wasomali wafanya maandamano dhidi ya al-Shabab baada ya shambulizi kali la kwenye hoteli
Mamia ya Wasomali, wakiwemo maafisa wakuu wa serikali, wamefanya maandamano ya amani mjini Mogadishu, Somalia, ili kulaani kundi la mrengo wenye itikadi kali za dini la al-Shabab kufuatia shambulizi kali la kwenye hoteli ya Lido Beach View lililosababisha vifo vya watu 37.
Wakikusanyika katika eneo la hoteli hiyo, waandamanaji walikuwa wamebeba mabango ya kuipinga al-Shabab na kulaani ukatili wa kundi hilo. Huku wakitamka kauli mbiu za kukemea na kuchukizwa na al-Shabab, waandamanaji hao pia walionyesha mshikamano wao kwa watu waliouawa na wengine 247 waliojeruhiwa katika shambulizi hilo.
Miongoni mwa waandamanaji hao walikuwepo manusura, mawaziri na maafisa walioapa kutotishwa na ugaidi na kuwataka Wasomali kuungana na kushirikiana na vyombo vya usalama kukabiliana na ugaidi.
Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika Kando Mbili za Mfereji Mkuu wa China Yaonyeshwa Mkoani Hebei
Michezo ya Kupanda Farasi ya"Agosti Mosi" yaanza katika Wilaya ya Litang Mkoa wa Sichuan, China
Mashindano ya kimataifa ya boti za matanga yamalizika huko Dalian, China
Watalii watembelea eneo lenye mandhari nzuri la Mlima Fairy la Chongqing, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma