Lugha Nyingine
Watu takriban 32 wauawa na wengine 107 kujeruhiwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha nchini Sudan
Picha iliyopigwa Julai 26, 2024 ikionyesha watu wakiwa katika eneo lililokumbwa na mafuriko katika mji wa Kassala, mashariki mwa Sudan. (Picha na Mohamed Osman Al-Zain/Xinhua)
KHARTOUM - Watu takriban 32 wameuawa na wengine 107 kujeruhiwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi majuzi na mafuriko ambayo yamekumba majimbo kadhaa ya Sudan, Wizara ya Afya ya Sudan imetangaza jana Jumatatu.
"Majimbo saba yameathiriwa na mvua na mafuriko, na nyumba 5,575 zimebomolewa," Al-Fadil Mohamed Mahmoud, mkurugenzi wa idara kuu ya dharura ya afya chini ya wizara hiyo, amesema katika taarifa.
Amesema kuwa mvua hiyo kubwa na mafuriko yamesababisha visa vingi vya kuhara vibaya , huku wagonjwa 102 wakiripotiwa katika jimbo la Kassala, wanne katika jimbo la Khartoum, na 16 katika jimbo la Gezira.
Amesema, hali ya afya ya watu katika majimbo mengine ni shwari, na wizara hiyo inafuatilia na kutumia hatua muhimu za kukabiliana na milipuko ya magonjwa ya msimu wa mvua.
Katika ripoti ya awali, Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Sudan ilikuwa ikikadiria kuwa kiwango cha maji ya Mto Gash kitapanda juu, mto huo ambao unapita Kassala, mji mkuu wa jimbo la Kassala. Wananchi wametakiwa kuwa waangalifu na kukaa mbali na kando za mto huo wa msimu.
Mafuriko ni tukio la kila mwaka nchini Sudan, kwa kawaida hutokea kati ya Juni na Oktoba. Katika miaka mitatu iliyopita, mvua kubwa zilizonyesha zimesababisha vifo vya mamia ya watu na kuharibu maeneo makubwa ya ardhi ya kilimo.
Msimu wa mvua wa mwaka huu umezidisha hali ngumu inayowakabili wale walioathiriwa na mgogoro unaoendelea kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na Kikosi cha Utoaji msaada wa Haraka (RSF).?
Picha iliyopigwa Julai 26, 2024 ikionyesha watu wakiwa katika eneo lililokumbwa na mafuriko katika mji wa Kassala, mashariki mwa Sudan. (Picha na Mohamed Osman Al-Zain/Xinhua)
Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika Kando Mbili za Mfereji Mkuu wa China Yaonyeshwa Mkoani Hebei
Michezo ya Kupanda Farasi ya"Agosti Mosi" yaanza katika Wilaya ya Litang Mkoa wa Sichuan, China
Mashindano ya kimataifa ya boti za matanga yamalizika huko Dalian, China
Watalii watembelea eneo lenye mandhari nzuri la Mlima Fairy la Chongqing, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma