Lugha Nyingine
China yatoa wito kwa ICC kuheshimu kikamilifu mamlaka ya mahakama na masuala halali ya Sudan
UMOJA WA MATAIFA - Dai Bing, naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) siku ya Jumatatu kuheshimu kikamilifu mamlaka ya mahakama na masuala halali ya Sudan wakati wa kushughulikia kesi ya Darfur.
"China imekuwa ikifuatilia kwa karibu uchunguzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kuhusu hali ya Darfur," amesema Balozi Dai katika hotuba yake kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ICC Sudan.
Balozi Dai amesema China inakaribisha rejea ya mwendesha mashtaka katika ripoti yake kwa ushirikiano wa serikali ya Sudan na mwendesha mashtaka kuhusu kesi ya Darfur, kutoa viza kwa timu ya mashtaka, na kujibu maombi kadhaa ya usaidizi.
Wakati wa kushughulikia kesi kwenye nyaraka zake, ICC inapaswa kuendelea kuongozwa na Mkataba wa Roma na mamlaka ya Baraza la Usalama, kuzingatia kikamilifu kanuni ya kukamilishana, kutekeleza mamlaka yake kwa kujitegemea, bila upendeleo, bila kutegemea upande wowote, na kwa mujibu wa sheria, na "kuheshimu kikamilifu mamlaka ya mahakama na masuala halali ya Sudan," amesema.
Balozi Dai amesisitiza kuwa China siku zote imekuwa ikihimiza suluhu ya kisiasa, ambayo ni "njia pekee inayowezekana ya kumaliza mgogoro na kurejesha amani," akibainisha kuwa mazungumzo ya hivi karibuni huko Geneva kati ya pande mbili za mgogoro na mpango wa kurudisha wapatanisha Djibouti yameundwa kasi nzuri kwa upatanishi na diplomasia ya kimataifa.
"Jumuiya ya kimataifa inapaswa kutoa kipaumbele kutumia zana za kisiasa na kidiplomasia zilizopo ipasavyo ili kuhimiza pande zote kuwa na mazungumzo zaidi, kutatua tofauti zao ipasavyo, na kupunguza mivutano mpaka mapigano yatasimamishwa kikamilifu," mjumbe huyo wa China amesema.
Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika Kando Mbili za Mfereji Mkuu wa China Yaonyeshwa Mkoani Hebei
Michezo ya Kupanda Farasi ya"Agosti Mosi" yaanza katika Wilaya ya Litang Mkoa wa Sichuan, China
Mashindano ya kimataifa ya boti za matanga yamalizika huko Dalian, China
Watalii watembelea eneo lenye mandhari nzuri la Mlima Fairy la Chongqing, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma