Lugha Nyingine
Rais Zelensky athibitisha kuwasili kwa Ndege za Kivita za F-16 nchini Ukraine
Mtu akitazama ndege ya kivita ya F16 kwenye Maonyesho ya Ulinzi wa Bahari Nyeusi na Mambo ya Anga mjini Bucharest, Romania, Mei 16, 2018. (Xinhua/Cristian Cristel)
KIEV - Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amethibitisha jana siku ya Jumapili kuwa ndege za kivita za F-16 zilizokuwa zikisubiriwa kwa muda mrefu zimewasili Ukraine, akisema "F-16 nchini Ukraine. Tumehakikisha hili," kwenye ujumbe wake alioandika kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram.
Marubani wa Ukraine tayari wameanza kutumia ndege ya F-16, amesema, bila kubainisha ni ndege ngapi zimetolewa kwa Ukraine.
Zelensky amezishukuru nchi za Denmark, Uholanzi, Marekani na washirika wengine wa Ukraine kwa kukubali ombi la Ukraine la kununua ndege hizo za kivita za F-16.
Vyombo vya habari vya Magharibi vimeripoti kwamba Ukraine ilipokea ndege 10 za kwanza za kivita za F-16 siku ya mwisho ya mwezi uliopita wa Julai.
Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika Kando Mbili za Mfereji Mkuu wa China Yaonyeshwa Mkoani Hebei
Michezo ya Kupanda Farasi ya"Agosti Mosi" yaanza katika Wilaya ya Litang Mkoa wa Sichuan, China
Mashindano ya kimataifa ya boti za matanga yamalizika huko Dalian, China
Watalii watembelea eneo lenye mandhari nzuri la Mlima Fairy la Chongqing, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma