Lugha Nyingine
China yalenga kuhimiza ushirikiano wa BRI kuendelezwa kwenye kiwango cha juu kwa ajili ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa nchi zote
BEIJING - China ingependa kuhimiza ushirikiano wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) kuendelezwa kwenye kiwango cha juu ili kusukuma mbele maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa nchi mbalimbali, na kujenga Dunia ya ufunguaji mlango na jumuishi, na iliyo ya mafungamano na kupata maendeleo kwa pamoja, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian amesema.
Lin amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi alipoulizwa kuhusu maendeleo na mafanikio ya hivi karibuni ya ushirikiano katika ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.
Lin amesema China imekuwa ikifanya kazi na pande mbalimbali katika zaidi ya miaka 10 iliyopita ili kuendeleza ushirikiano katika ujenzi wa pamoja wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na China, pamoja na pande nyingine zinahimiza ujenzi huo kustawi na kuleta manufaa kwa watu na nchi mbalimbali duniani, zikiifanya BRI kuwa bidhaa ya umma ya kupokelewa duniani na kuwa jukwaa la ushirikiano la ufunguaji mlango na ujumuishaji, la kunufaishana na kupata maendelo kwa pamoja.
“Katika zaidi ya miaka 10 iliyopita, ushirikiano wa ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja siyo tu umehimiza mawasiliano zaidi kati ya watu na mzunguko mzuri wa usambazaji bidhaa, bali pia kuwafanya watu wa nchi husika wajisikia majivuno na furaha zaidi” amesema Lin.
Amesema China imetia saini nyaraka za ushirikiano wa BRI na nchi zaidi ya 150 na mashirika zaidi ya 30 ya kimataifa, na mwaka jana, biashara ya China na nchi washirika ilifikia thamani ya yuan trilioni 19.5 (dola za kimarekani karibu trilioni 2.74), sawa na ongezeko la asilimia 2.8, ikichukua asilimia 46.6 ya jumla ya kiasi cha uagizaji na uuzaji nje bidhaa, ikiweka rekodi mpya kwa ukubwa na sehemu tangu kutolewa kwa pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.
"Tunaendelea kuwa na dhamira katika ufunguaji mlango na kushirikiana kwa mustakabali wa pamoja wa siku za baadaye," Lin amesema, akiongeza kuwa China ingependa kufanya ushirikiano na pande zote na kuungana mkono, kwa kupitia mawasiliano zaidi na kufundishana kuimarisha "mafungamano” ya miundombinu, kuweka kanuni za umakini zaidi na vigezo vya juu zaidi, na kuimarisha mawasiliano ya kitamaduni.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma