Lugha Nyingine
Libya yaandaa Jukwaa la Wahamiaji Kuvuka Bahari ya Mediterania
Waziri Mkuu wa Libya Abdul-Hamed Dbeibah (katikati) akitoa hotuba kwenye mkutano wa Jukwaa la Wahamiaji Kuvuka Bahari ya Mediterania huko Tripoli, Libya, Julai 17, 2024. (Picha na Hamza Turkia/Xinhua)
TRIPOLI - Viongozi wa Ulaya na Afrika wamekusanyika nchini Libya siku ya Jumatano kuhudhuria kwenye mkutano wa Jukwaa la Wahamiaji Kuvuka Bahari ya Mediterania katika juhudi za kushirikiana kutafuta suluhu juu ya suala la uhamiaji ambapo jukwaa hilo linalenga kupata matarajio ya pamoja ambayo yataongeza ushirikiano na uratibu kati ya nchi husika, ili kuendeleza misingi ya uhusiano endelevu wa kiuchumi na kibiashara kati ya Ulaya na Afrika, amesema Waziri Mkuu wa Libya Abdul-Hamed Dbeibah.
Dbeibah ametoa wito wa kuelekeza upya fedha zinazotumika kwa sasa kudhibiti uhamiaji usio wa kawaida kwenda katika kufadhili miradi ya maendeleo katika nchi chanzo cha wahamiaji za Afrika, Shirika la Habari la kiserikali la Libya, LANA limeripoti.
“Tutekeleze miradi halisi yenye kuleta utulivu wa wananchi wa nchi hizi katika kanda zao,” amesema.
Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby Itno amehimiza maendeleo ya ufumbuzi wa uhamiaji usio wa kawaida na kuchunguza sababu zake, akisisitiza umuhimu wa kulinda haki za binadamu na wakati huo huo kushughulikia suala hili.
Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni amesema kuwa nchi yake inatoa kipaumbele kwa kutatua suala la uhamiaji, akibainisha kuwa wahamiaji wengi wasio wa kawaida wanahitaji kuimarishwa juhudi pamoja na nchi za kanda husika.
Waziri Mkuu wa Malta Robert Abela amezungumzia juhudi zinazofanywa na serikali ya Libya kwa kuokoa wahamiaji na kufanya ushirikiano katika suala la uhamiaji usio wa kawaida, akitoa wito wa kuchukua hatua za pamoja za kupunguza uhamiaji na mitandao ya uhalifu wa kupangwa.
Shirika la Habari la LANA limesema, mkutano huo utashughulikia masuala kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuimarisha usimamizi wa mpaka, kuimarisha mifumo ya uokoaji na msaada kwa wahamiaji, na kutoa uungaji mkono unaohitajika kwa nchi zinazopokea wahamiaji.
Tangu kuangushwa kwa kiongozi wa zamani Muammar Gaddafi mwaka wa 2011, Libya imekuwa mahali pendwa pa kuondokea kwa baadhi ya wahamiaji wa Afrika wanaojaribu kuvuka Bahari ya Mediterania hadi kufikia mwambao wa Ulaya.
Washiriki wakihudhuria kwenye mkutano wa Jukwaa la Wahamiaji Kuvuka Bahari ya Mediterania huko Tripoli, Libya, Julai 17, 2024. (Picha na Hamza Turkia/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma