Lugha Nyingine
China na?nchi za Latini Amerika zaingiza kasi kwenye maendeleo ya kimataifa katika muongo mmoja uliopita
Abiria wa safari ya kwanza ya ndege ya moja kwa moja inayounganisha miji ya Shenzhen, kusini mwa China na Mexico City, mji mkuu wa Mexico, wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Benito Juarez mjini Mexico City, Mexico, Mei 11, 2024. (Xinhua/Li Mengxin)
MEXICO CITY - Tangu Rais Xi Jinping wa China apendekeze kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Nchi za Latini Amerika na Karibiani (LAC), muongo mmoja umepita, ambapo katika kipindi hicho ushirikiano kati ya China na nchi za LAC umebadilika kutoka kuwa dira hadi hatua, kutoka mpango hadi kuwa uhalisia.
China na nchi za LAC ni nguvu za kiujenzi za usimamizi wa kimataifa. Katika kipindi kipya cha sasa cha misukosuko na mageuzi, Dunia inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo mgogoro wa Ukraine na vita kati ya Palestina na Israel.
Mwezi Mei, China na Brazil zilifikia makubaliano ya pamoja juu ya suluhu ya kisiasa ya mgogoro wa Ukraine, zikitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kwa pamoja kuchukua jukumu la kiujenzi katika kupunguza mgogoro huo na kuendeleza mazungumzo ya amani.
Kuhusu uongozi wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi, China imenufaika uzoefu wake wa maendeleo endelevu na ulinzi wa mifumo ikolojia ya baharini na nchi za Karibiani. Pia imewekeza katika upanuzi wa uwezo wa nishati mbadala na katika miradi ya miundombinu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na hivyo kuboresha ustawi wa wakazi wa eneo hilo.
Kuhusu kupunguza umaskini, China imehamisha teknolojia ya hali ya juu ya kilimo kwa nchi za Karibiani kama Antigua na Barbuda, Dominica na nyinginezo, ikitoa mfano wa ushirikiano wenye usawa kati ya nchi kubwa na ndogo na kusaidia wakulima wenyeji kuongeza mapato yao.
China na nchi za LAC ni nguvu zinazohamasisha ushirikiano na maendeleo. Kuanzia ujenzi wa miundombinu hadi biashara hadi nyanja zinazoibuka za kisayansi na kiteknolojia pande hizo mbili zimekuwa zikishirikiana kwa ukaribu.
Nchi jumla ya 22 za LAC zimejiunga na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) kwa kutia saini mikataba tofauti ya ushirikiano. China na nchi za LAC pia ni nguvu za kusukuma mawasiliano kati ya ustaarabu tofauti.
Msemo wa Latini Amerika unasema, "Njia pekee ya kunufaisha faida ni kuwa mkarimu kwa wote." Hivi sasa, China inahimiza kwa nguvu kubwa ujenzi wa mambo ya kisasa, huku nchi za LAC zikilenga kuendeleza vichocheo vipya vya ukuaji wa uchumi.
Pande hizo mbili zinaimarisha ushirikiano kwa msingi thabiti, na kuendeleza kwa pamoja ujenzi wa jumuiya ya China na LAC yenye mustakabali wa pamoja.
Waziri Mkuu wa Trinidad na Tobago Keith Rowley (wa kwanza kulia), Waziri wa Biashara na Viwanda Paula Gopee-Scoon (wa tatu kushoto), Balozi wa China nchini Trinidad na Tobago Fang Qiu (wa pili kushoto) na maafisa wengine wakihudhuria hafla ya uzinduzi wa Eneo Maalum la Viwanda la Phoenix huko Joint Lisas, bandari ya pili kwa ukubwa Trinidad na Tobago, Januari 10, 2024. (Xinhua/Zhu Wanjun)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma