Lugha Nyingine
Kura ya maoni yaonesha wapiga kura wanne kati ya watano wana wasiwasi Marekani inaelekea nje ya udhibiti baada ya Trump kupigwa risasi
Mwanamke akitembelea uwanja wa National Mall mjini Washington, D.C., Marekani, tarehe 29 Machi 2022. (Xinhua/Liu Jie)
NEW YORK - Wamarekani wanne kati ya watano wana wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa ghasia za kisiasa kufuatia jaribio la kumuua Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, na wanahofia kwamba Marekani "inaelekea nje ya udhibiti," kura ya maoni ya Reuters/Ipsos imeonesha siku ya Jumanne.
Trump alinusurika jaribio la kumwua kwenye mkutano wa kampeni huko Pennsylvania siku ya Jumamosi. Kupigwa risasi huko kuligeuka kuwa kichwa cha habari cha vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, na kupeleka mishtuko ya kisiasa kote nchini humo, ikiwa imebakia miezi zaidi ya mitatu kabla ya uchaguzi mkuu wa rais.
Asilimia 84 ya wapiga kura kwenye uchaguzi huo wamesema wana wasiwasi kwamba watu wenye mirengo ya itikadi kali watafanya vurugu baada ya uchaguzi wa Novemba, kiasi ambacho ni kubwa kuliko asilimia 74 ya matokeo ya awali ya Mei.
Asilimia takriban 80 ya wapiga kura wa Marekani, ikiwa ni pamoja na wanachama wa vyama vya Democrat na Republican, wanakubali kwamba "nchi inatoka nje ya udhibiti."
Ni asilimia 5 pekee ya waliohojiwa wamesema inakubalika kwa mtu katika chama chake cha kisiasa kufanya vurugu ili kufikia lengo la kisiasa, ikiwa ni chini kutoka asilimia 12 ya maoni ya Reuters/Ipsos kuanzia Juni 2023.
Kwa mujibu wa kura hiyo ya maoni, mgombea wa rais wa chama cha Republican, Trump anaongoza kwa tofauti ndogo dhidi ya Rais Joe Biden wa Chama cha Democrat, akiwa na asilimia 43 dhidi ya 41.
Imeonekana kuwa jaribio hilo la kutaka kumuua Trump halijasababisha mabadiliko makubwa katika hisia za wapiga kura, Reuters imesema baada ya kura hiyo ya maoni.
Kura hiyo ya maoni iliyofanywa mtandaoni, imewahoji watu wazima 1,202 wa Marekani kote nchini humo, wakiwemo wapiga kura 992 waliojiandikisha.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma