Lugha Nyingine
35 wafariki dunia, 250 wajeruhiwa katika mafuriko yaliyotokea mashariki mwa Afghanistan
Watu wakiangalia uharibifu baada ya mafuriko makubwa katika Wilaya ya Surkh Rod, Jimbo la Nangarhar, Afghanistan, tarehe 15 Julai 2024. (Picha na Aimal Zahir/Xinhua)
JALALABAD, Afghanistan - Watu takriban 35 wamefariki dunia na wengine 250 kujeruhiwa wakati mvua mkubwa na maporomoko ya mafuriko yalipokumba Jimbo la Nangarhar mashariki mwa Afghanistan siku ya Jumatatu alasiri, alisema ofisa wa eneo hilo. Na aliongeza kuwa, mkurugenzi wa habari na utamaduni wa Nangarhar, Qurishi Badlon amesema, maafa hayo yameathiri mji mkuu wa Jimbo la Jalalabad, Wilaya ya Sukh Rod na maeneo ya jirani katika jimbo hilo linalopakana na Pakistan.
Idadi ya vifo na majeruhi huenda itaongezeka, ofisa huyo ameongeza.
Maafa kama hayo ya asili pia yamegharimu maisha ya watu watano katika jimbo jirani ya Kunar la Nangarhar saa za mapema Jumatatu asubuhi.
Mvua kubwa na mafuriko yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 400 na kusababisha maelfu ya watu kupoteza makazi yao tangu mwezi Mei katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita.
Watu wakiangalia uharibifu baada ya mafuriko makubwa katika Wilaya ya Surkh Rod, Jimbo la Nangarhar, Afghanistan, tarehe 15 Julai 2024. (Picha na Aimal Zahir/Xinhua)
Watu wakiangalia uharibifu baada ya mafuriko makubwa katika Wilaya ya Surkh Rod, Jimbo la Nangarhar, Afghanistan, tarehe 15 Julai 2024. (Picha na Aimal Zahir/Xinhua)
Watu wakiwa wamekaa kwenye vifusi vya nyumba iliyobomolewa baada ya mafuriko makubwa katika Wilaya ya Surkh Rod, Jimbo la Nangarhar, Afghanistan, tarehe 15 Julai 2024. (Picha na Aimal Zahir/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma