久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Mpango wa michezo wawezesha vijana wanaoishi katika mazingira magumu nchini Namibia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 15, 2024

Makocha wakipiga picha katika Shule ya Sanaa ya Mpira wa Kikapu mjini Windhoek, mji mkuu wa Namibia, Julai 12, 2024. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua)

Makocha wakipiga picha katika Shule ya Sanaa ya Mpira wa Kikapu mjini Windhoek, mji mkuu wa Namibia, Julai 12, 2024. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua)

WINDHOEK - Vijana wengi kutoka maeneo ya watu wenye kipato cha chini katika kitongoji cha Katutura huko Windhoek, mji mkuu wa Namibia, wanakumbana na ukosefu wa vifaa na mara nyingi hujihusisha na shughuli hatari za kijamii, hata hivyo, Shule ya Sanaa ya Mpira wa Kikapu (BAS) iliyoanzishwa na mtaalam wa mpira wa kikapu wa Ujerumani Frank Albin Mwaka 2010, amewezesha vijana hao wenyeji kupitia michezo.

Meneja wa BAS Malakia Mathias amesema mpango huo ambao ni mradi usio na faida wa baada ya muda wa masomo unachanganya mpira wa kikapu na elimu ili kuwafundisha stadi za maisha na kuwawezesha.

BAS hutoa huduma ya baada ya masomo, mafunzo katika hesabu na Lugha ya Kiingereza, kozi za ujuzi wa matumizi ya kompyuta, mafunzo ya mpira wa vikapu, na kuandaa mashindano ya kutamka maneno. Shule hiyo ilipata umaarufu zaidi na kuanzisha kituo chake katika eneo la Katutura Mwaka 2015.

"Njia yetu ya kipekee ni elimu kwanza juu ya mpira wa kikapu ili kusaidia vijana kushinda changamoto za kijamii na kiuchumi na kuandaa njia kwa mustakabali mzuri wa baadaye," Mathias amesema Jumamosi.

Katika siku ya kawaida katika BAS, vijana kutoka shule zilizochaguliwa huko Katutura huja kituoni hapo wakati wa mchana, kula chakula, kupokea mafunzo, kucheza mpira wa kikapu, na kisha kurudi nyumbani. BAS kwa sasa inahudumia vijana zaidi ya 30.

Kwa mujibu wa Mathias, BAS inatumia mpira wa kikapu kushughulikia changamoto za kijamii kama vile mimba za utotoni, ushawishi mbaya, na matumizi mabaya ya dawa za kulevya yaliyoenea katika kitongoji chenye mazingira duni cha Katutura. Huduma zinatolewa na makocha wa kujitolea wa wenyeji na wa kimataifa ambao hujikita katika elimu, ujumuishaji wa ujuzi wa kijamii, na kuweka mazingira salama kwa mazungumzo ya wazi.

"Pia tunafanya kazi kwa karibu na shule za mitaa kufuatilia maendeleo na kuwatia moyo wanafunzi. Pia tunajumuisha teknolojia katika kujifunza," amesema.

Tangu kuanzishwa kwake, BAS imetoa mchango mzuri kwa maisha ya vijana zaidi ya 900.

Salmi Ndipo, ambaye ni mnufaika mwenye umri wa miaka 12, ameipongeza shule hiyo kubadilisha maisha yake kwa mwaka mmoja tu.

"Kabla ya hili, ningeweza kuathiriwa vibaya na wenzangu. Kutoka kwenye mpira wa kikapu na huduma hapa, nimepata kujiamini na nidhamu, na kusababisha kuimarika kwa ufaulu wa kitaaluma," amesema.

Waziri wa Elimu, Sanaa na Utamaduni wa Namibia, Ester Nghipondoka amesema mipango kama vile BAS imethibitishwa kusaidia utoaji wa elimu na kuleta maendeleo ya kielimu kwa vijana nchini humo.

Makocha wakipiga picha katika Shule ya Sanaa ya Mpira wa Kikapu mjini Windhoek, mji mkuu wa Namibia, Julai 12, 2024. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua)

Makocha wakipiga picha katika Shule ya Sanaa ya Mpira wa Kikapu mjini Windhoek, mji mkuu wa Namibia, Julai 12, 2024. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua)

Vijana wakijifunza kucheza mpira wa kikapu katika Shule ya Sanaa ya Mpira wa Kikapu mjini Windhoek, mji mkuu wa Namibia, Julai 12, 2024. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua)

Vijana wakijifunza kucheza mpira wa kikapu katika Shule ya Sanaa ya Mpira wa Kikapu mjini Windhoek, mji mkuu wa Namibia, Julai 12, 2024. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>