Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping akutana na Waziri Mkuu wa Vietnam Minh Chinh mjini Beijing
Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Juni 26, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amekutana na Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh siku ya Jumatano mjini Beijing, waziri mkuu huyo ambaye yuko China kuhudhuria Mkutano wa Davos wa Majira ya Joto 2024, ambapo Rais Xi amemwomba Chinh kufikisha salamu zake za dhati kwa Nguyen Phu Trong, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam, na kwa Rais wa Vietnam, To Lam.
Rais Xi amesema katika ziara yake nchini Vietnam mwishoni mwa mwaka jana, yeye na Trong walitangaza ujenzi wa jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja ambayo ni yenye umuhimu wa kimkakati, ikiingiza maendeleo ya uhusiano wa pande mbili katika kipindi kipya.
Amesema, katika kipindi cha nusu mwaka uliopita, vyama na nchi hizo mbili zimefurahia mawasiliano ya karibu kati ya viongozi wa ngazi za juu na ushirikiano mzuri katika sekta mbalimbali, na kuleta manufaa halisi kwa watu wa nchi hizo mbili.
Rais Xi amesema kuwa dunia ya leo inakabiliana na mabadiliko ambayo hayajawahi kuonekana katika miaka 100 iliyopita, China na Vietnam zimedumisha maendeleo ya haraka ya kiuchumi na utulivu wa jamii wa muda mrefu, na kuonyesha nguvu za mfumo wa ujamaa.
Amesema ujenzi wa jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja ambayo ni ina umuhimu wa kimkakati unaendana na mahitaji ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa nchi hizo mbili, na unasaidia kudumisha amani na utulivu wa kikanda na kuhimiza maendeleo ya mambo ya kijamaa duniani.
“China ingependa kujiunga pamoja na Vietnam katika kudumisha mshikamano na urafiki, kuimarisha kuungana mkono, na kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana” Rais Xi amesema, akiongeza kuwa China pia ingependa kushirikiana na Vietnam kusonga mbele kuelekea ujenzi wa mambo ya kisasa na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya amani na utulivu, maendeleo na ustawi wa Dunia.
Ameongeza kuwa, pande hizo mbili zinapaswa kushughulikia ipasavyo masuala ya bahari, kuharakisha maendeleo ya bahari kwa pamoja na kulinda kwa pamoja amani na utulivu wa kikanda.
Kwa upande wake Chinh amewasilisha salamu za dhati za Katibu Mkuu Nguyen Phu Trong na Rais To Lam kwa Rais Xi. Amesema Vietnam na China, zote zikiwa ni nchi za kijamaa zinazoongozwa na chama cha kikomunisti, zina desturi ya ujirani mwema na urafiki.
Akitoa pongezi kubwa kwa mafanikio makubwa ya China katika sekta mbalimbali, Chinh amesema upande wa Vietnam unasifu sana mchango muhimu wa China kama injini na nguzo ya ukuaji wa uchumi wa Dunia, na kuunga mkono maendeleo na ustawi wa China na kutimizwa kwa Lengo lake la Miaka 100 ya Pili kama ilivyopangwa.
Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Vietnam Pham Minh Chinh kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Juni 26, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma