Lugha Nyingine
Eneo la Katikati ya China laimarisha jukumu la kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Afrika
Watu wakinunua bidhaa kwenye Maonyesho ya tatu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika yaliyofanyika katika kituo cha kimataifa cha Mikutano na Maonyesho cha Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati ya China, Julai 1, 2023. (Xinhua/Chen Zhenhai)
CHANGSHA – Kwenye pwani ya Kenya, wavuvi walikuwa wakitupa nyavu zao baharini, wakivua dagaa mwitu. Kitu ambacho hawakuwa wakijua hata kidogo, ni kwamba samaki hao wangeanza safari ya kuelekea China, ambako wangetengenezwa kuwa chakula kitamu kitakachouzwa kwa maduka makubwa katika nchi zaidi ya 30.
Kampuni ya Vyakula ya Jinzai katika Mkoa wa Hunan katikati ya China inaendesha shughuli hii ya kimataifa. Tangu Mwaka 2022, baada ya bidhaa za majini za Kenya kupata soko la China, kampuni hiyo imeibuka kuwa moja ya waagizaji wakubwa wa bidhaa hizi.
"Thamani ya Mauzo ya samaki wadogo wa kina kirefu baharini waliokaushwa ya kampuni hiyo, imezidi yuan bilioni 1 (karibu dola za kimarekani milioni 140) na makumi ya maelfu ya tani za samaki waliagizwa kutoka nje kila mwaka," amesema Zhou Jinsong, mwenyekiti wa kampuni hiyo.
Kampuni ya Jinzai inatoa mfano wa mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara yanayostawi kati ya Hunan na Afrika. Mkoa huo umekaa mstari wa mbele katika uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika. Ikitumia teknolojia ya hali ya juu ya kilimo, utengenezaji wa vifaa na ujenzi wa miundombinu, Hunan imedumisha kiwango cha ukuaji wa uchumi wa kila mwaka cha asilimia 23.1 katika ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na Afrika, takwimu rasmi zinaonesha.
Mbali na Hunan, mikoa mingine matano ya katikati ya China, imehimizwa kuanzisha mageuzi ya ndani na ufunguaji wa nyanda za juu. Eneo hilo litaharakisha maendeleo ya majukwaa kama vile eneo la majaribio la kuzidisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika, kama ilivyobainishwa kwenye mkutano na waandishi wa habari mwezi wa Mei na Wizara ya Biashara ya China.
Kwa kuongozwa na mkakati wa kitaifa, mikoa ambayo yaliyoko mbali na mipaka na bahari, yanaendesha kikamilifu uvumbuzi wa kiutaratibu na wenye matokeo halisi katika ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na Afrika.
Maonesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika, yanayofanyika kila baada ya muda fulani huko Changsha, mji mkuu wa Hunan, yamekuwa maonyesho muhimu kwa bidhaa za kilimo za Afrika, na hivyo kuongeza mwonekano wao kimataifa.
Kwenye Jengo la Makao Makuu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika jijini humo, wenyeji kutoka pande zote mbili waliuza bidhaa za Afrika kupitia utangazaji wa moja kwa moja mtandaoni ili kusaidia kupata mauzo mazuri katika masoko ya China na kimataifa. Likiwa na ukubwa wa mita za mraba 100,000, jengo hilo lilianza kufanya kazi katikati ya Juni mwaka huu na linatarajiwa kufikia kiwango cha biashara kati yake na Afrika kinachofikia jumla ya Yuan bilioni 30 katika miaka mitatu ijayo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma