久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Mamia ya watu wanufaika na kambi ya matibabu iliyoandaliwa na kampuni kubwa ya mafuta ya China nchini?Uganda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 21, 2024

Daktari kutoka timu ya madaktari wa China nchini Uganda akimchunguza mtoto kwenye kambi ya matibabu iliyoandaliwa katika Wilaya ya Kikuube, Magharibi mwa Uganda, Juni 19, 2024. (Picha na Tian Yu/Xinhua)

Daktari kutoka timu ya madaktari wa China nchini Uganda akimchunguza mtoto kwenye kambi ya matibabu iliyoandaliwa katika Wilaya ya Kikuube, Magharibi mwa Uganda, Juni 19, 2024. (Picha na Tian Yu/Xinhua)

KAMPALA - Kampuni kubwa ya mafuta ya China, China National Offshore Oil Corporation (CNOOC) nchini Uganda imeandaa kambi ya matibabu ya siku mbili katika Wilaya ya Kikuube, Magharibi mwa Uganda ambapo mamia ya wakazi wa eneo hilo wamepatiwa huduma za afya na tiba bila malipo.

Taarifa iliyotolewa na CNOOC tawi la Uganda siku ya Jumatano imesema kambi hiyo ya matibabu, ambayo ilianza Jumatano na kuhitimishwa jana Alhamisi, imeandaliwa kwa kushirikiana na timu ya madaktari wa China nchini Uganda, ambayo inajumuisha madaktari na wataalam 20.

Watu takriban 1,000 walikuwa wakitarajiwa kunufaika na kambi hiyo ya matibabu.

Ikiwa imefanyika chini ya kaulimbiu ya "Wezesha Afya, Kumbatia Maisha," kambi hiyo imetoa huduma za upimaji na uchunguzi wa afya, ushauri, tiba na elimu ya afya bila malipo kwa wakazi wa eneo hilo, hasa wanawake na watoto.

"Kambi ya matibabu imetibu magonjwa ya kuambukiza kama vile malaria, typhoid, kaswende, homa ya ini B, na VVU, pamoja na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwa ni pamoja na shinikizo la damu, kisukari, saratani ya mlango wa kizazi, na vidonda vya tumbo," kampuni hiyo imesema katika taarifa yake.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kampuni hiyo ya CNOOC na timu ya madaktari wa China pia wamekabidhi dawa na vifaa vya watoto kwa moja ya vituo vya afya vya eneo hilo.

Liu Xiangdong, Mkuu wa CNOOC Tawi la Uganda, amesema kambi hiyo ya matibabu inadhihirisha dhamira ya kampuni hiyo katika kuimarisha uhusiano kati ya China na Uganda.

"Kupitia mipango kama hii, tunalenga kutoa mchango kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Uganda na kuimarisha urafiki kati ya nchi zetu mbili tunaposhughulikia nishati kwa maisha bora ya baadaye," amesema.

Vincent Alpha, makamu mwenyekiti wa Wilaya ya Kikuube, ameipongeza timu hizo kwa kuendelea kuwaunga mkono wenyeji. "Tunaishukuru sana CNOOC tawi la Uganda kwa uungaji mkono wake na dhamira yao isiyoyumba kwa afya na ustawi wa jamii yetu," Alpha amesema.

Daktari kutoka timu ya madaktari wa China nchini Uganda akimpima mkaazi kwenye kambi ya matibabu iliyoandaliwa katika Wilaya ya Kikuube, Magharibi mwa Uganda, Juni 19, 2024. (Picha na Tian Yu/Xinhua)

Daktari kutoka timu ya madaktari wa China nchini Uganda akimpima mkaazi kwenye kambi ya matibabu iliyoandaliwa katika Wilaya ya Kikuube, Magharibi mwa Uganda, Juni 19, 2024. (Picha na Tian Yu/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>