Lugha Nyingine
Ripoti juu ya viwanda vya?NEVs vya China barani Ulaya yazinduliwa Brussels
Mkuu wa Shirika la Habari la China, Xinhua Fu Hua akihutubia hafla ya uzinduzi wa ripoti inayoangazia viwanda vya magari yanayotumia nishati mpya (NEVs) vya China barani Ulaya na Jopo la Wakurugenzi Watendaji Wakuu wa Ulaya na China mjini Brussels, Ubelgiji, Juni 19, 2024. (Xinhua/Peng Ziyang)
BRUSSELS –Idara ya Habari za Kiuchumi ya China ya Shirika la Habari la China, Xinhua na Shirikisho la Wafanyabiashara wa China katika Umoja wa Ulaya zimezindua kwa pamoja ripoti inayoangazia viwanda vya magari yanayotumia nishati mpya (NEV) vya China barani Ulaya siku Jumatano.
Ripoti hiyo iliyopewa jina la "Kuifanya Ulaya iwe ya Kijani - Ripoti ya Maendeleo ya Viwanda vya NEV vya China barani Ulaya" imezinduliwa pembezoni mwa Jopo la Maofisa Watendaji Wakuu wa Ulaya na China lililofanyika Brussels.
Akihutubia kwenye hafla hiyo, Mkuu wa Xinhua, Fu Hua amesema China na Ulaya zina uwezo wa kufikia ushirikiano wa kunufaishana katika sekta ya magari yanayotumia nishati mpya (NEV), kutokana na dhamira yao ya kuhimiza uhifadhi wa nishati, kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni na kuishi kwa mapatano kati ya binadamu na mazingira asilia.
Shirika la Habari la China, Xinhua limetoa mfululizo wa ripoti za habari zinazofuatiliwa na watu wengi kuhusu maendeleo ya sekta ya NEV ya China na ushirikiano kati ya China na Ulaya katika sekta ya NEV, Fu amesema.
Ripoti hiyo iliyotolewa Jumatano imechambua mahitaji ya kimataifa ya NEVs na majumuisho ya maendeleo na faida za ushindani wa sekta ya NEV ya China, ikitoa marejeleo muhimu kwa China na Ulaya ili kuimarisha ushirikiano wa teknolojia, mawasiliano kuhusu sera, ushirikiano wa ugavi na uwekezaji, amesema.
Akiuita uongozi wa China katika sekta ya kuondoa kaboni "njia inayoweza kufuata," Msaidizi wa zamani wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Brice Lalonde amesema China imekusanya mafanikio ya tija katika sekta ya NEV na kufunika hatua zote muhimu katika sekta hii.
Mtu akitazama aina jipya la gari linalotumia nishati mpya la Kampuni ya magari ya IM kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Magari ya Beijing Mwaka 2024 mjini Beijing, China, Aprili 30, 2024. (Xinhua/Zhang Chenlin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma