Lugha Nyingine
Rais Xi asisitiza utii wa kisiasa wa PLA kwenye mkutano muhimu uliofanyika katika kituo cha zamani cha mapinduzi
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa Kazi ya Kisiasa wa CMC mjini Yan'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China, Juni 17, 2024. (Xinhua/Li Gang)
YAN'AN, Shaanxi - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amesisitiza utii wa kisiasa wa vikosi vya jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) wakati mkutano muhimu juu ya kazi ya kisiasa katika jeshi hilo ukifanyika katika Mji wa Yan'an, ambapo ni kituo cha zamani cha mapinduzi cha China katika Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China.
Rais Xi ameagiza kufanya juhudi za kuhakikisha uhakikisho thabiti wa kisiasa kwa kujenga jeshi lenye nguvu, alipokuwa akihutubia Mkutano wa Kazi ya Kisiasa wa CMC, uliofanyika Jumatatu hadi Jumatano.
Mkutano huo wa Yan'an, ambao Rais Xi ameamua mwenyewe kuuitisha, umefanyika miaka 10 baada ya mkutano kama huo kufanyika mjini Gutian, Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China. Washiriki wamejadili na kupanga mipango ya kuhimiza kazi za kisiasa ndani ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA).
Rais Xi amesisitiza kuwa ni lazima kushikilia uongozi kamili wa Chama juu ya jeshi na kujenga kikosi cha maofisa wa kijeshi wenye sifa nzuri ya juu walio watiifu, wafuata maadili, wanaowajibika, na wenye uwezo wa kubeba majukumu ya kujenga jeshi lenye nguvu.
Siku ya Jumatatu alasiri, Rais Xi aliongoza maofisa wa CMC na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali kutembelea kituo cha zamani cha mapinduzi cha Wangjiaping, ambako ni yaliko makao makuu ya CMC kuanzia Agosti 1937 hadi Machi 1947.
Rais Xi alitembelea makaazi ya zamani ya viongozi marehemu wa mapinduzi wakiwemo Mao Zedong, Zhou Enlai na Zhu De mjini Yan'an ili kukumbuka mapambano yao kwa ajili ya mapinduzi.
“Mkutano wa Yan'an ni alama ya kurejea kwenye nia ya awali kwa jeshi,” Rais Xi amesema.
Amewataka maofisa waandamizi wa jeshi kubeba majukumu waliyokabidhiwa na Chama na wananchi, na kuendelea kuimarisha jeshi siku hadi siku.
Rais Xi ametoa hotuba muhimu kwenye mkutano huo, akibainisha kuwa baada ya Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC Mwaka 2012, Kamati Kuu ya CPC ilifanya mkutano wa kazi ya kisiasa wa kijeshi Mwaka 2014 huko Gutian na kuboresha utendaji na mwenendo wa kisiasa kupitia marekebisho ya vitendo na mienendo ya kazi mbalimbali za chama.
“Hatua za kusimamia jeshi kwa nidhamu kali zimetekelezwa kikamilifu kwa dhamira na nguvu isiyo na kifani, na kufikia mafanikio ya kihistoria katika kuimarisha utii wa kisiasa jeshini,” amesema Rais Xi.
Amesisitiza kuwa kazi ya kisiasa daima ni uhai wa jeshi la nchi, na jeshi hilo lazima liongozwe na wale wanaoaminika na kutegemeka na watiifu kwa Chama, na kabisa kusiwe na nafasi ya ufisadi ndani ya jeshi.
Rais Xi Jinping wa China akiongoza maofisa wa CMC na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali kutembelea kituo cha zamani cha mapinduzi huko Wangjiaping katika Mji wa Yan'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China, Juni 17, 2024. (Xinhua/Li Gang)
Rais Xi Jinping wa China akikutana na washiriki wa Mkutano wa Kazi ya Kisiasa wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) mjini Yan'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa wa China, Juni 17, 2024. (Xinhua/Li Gang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma