Lugha Nyingine
Zimbabwe yachukua hatua ya kukabiliana na uhaba wa sarafu mpya ya ZiG
Mtu akionyesha sarafu mpya ya Zimbabwe Gold mjini Harare, Zimbabwe, tarehe 15 Mei 2024. (Picha na Shaun Jusa/Xinhua)
HARARE - Benki kuu ya Zimbabwe imechukua hatua kuepusha uhaba wa sarafu ya nchi hiyo, Zimbabwe Gold (ZiG), ambayo ilizinduliwa Aprili 5 mwaka huu kwa ajili ya kukabiliana na mfumuko wa bei na kuleta utulivu wa sarafu, huku kukiwa na wasiwasi kwamba uhaba huo unatatiza maisha ya kila siku za watu.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa siku ya Jumatano, Gavana wa Benki Kuu ya Zimbabwe (RBZ) John Mushayavanhu amesema benki hiyo imetelekeza mpango katika kitengo chake cha huduma za kifedha, Homelink, ili kuwezesha wananchi wanaofanya miamala kubadili sarafu ya Zimbabwe kwa noti za thamani ya ZiG1, ZiG2, ZiG5, na ZiG10.
Thamani hiyo ndogo inalenga kuwapa chenji wananchi wanaofanya miamala huku benki kuu hiyo, ikishikilia noti za ZiG20, ZiG50, ZiG100, na ZiG200 wakati inapojaribu kuzuia soko sambamba na kupunguza mfumuko wa bei.
Takwimu zilizotolewa na Shirika la Kitaifa la Takwimu la Zimbabwe Mei 29 zinaonyesha kuwa bei ya wanunuzi bidhaa imeshuka kwa asilimia 2.4 kuanzia Aprili. Hali hiyo inatokana na kuzinduliwa kwa ZiG Aprili 5 ikiwa ni sehemu ya hatua za kuimarisha uthabiti wa viwango vya ubadilishaji fedha na kudhibiti mfumuko wa bei.
Mushayavanhu amesema RBZ imejidhatiti kuhakikisha mzunguko wa fedha wa ndani wa kutosha ili kusaidia shughuli za kawaida za biashara na shughuli za kiuchumi.
"Benki inatoa wito kwa watu wote, wasafiri, waendeshaji wa usafiri wa umma, wauzaji reja reja, wafanyabiashara wasio rasmi na umoja wao, jumuiya ya wauzaji bidhaa ndogo ndogo, na wadau wengine wakuu wanaokutana ana kwa ana na umma unaofanya miamala, kukaribia tawi lao la karibu la Homelink na kubadilisha kwenda fedha taslimu za ZiG kwa kutumia kadi za benki au mkopo kuanzia Juni 10," amesema.
Ameongeza kuwa fedha za kigeni pia zinaweza kubadilishwa kwa ZiG katika matawi yale yale ya Homelink.
Watu wakiwa kwenye foleni ili kutoa sarafu mpya ya Zimbabwe Gold nje ya benki moja mjini Harare, Zimbabwe, tarehe 30 Aprili 2024. (Picha na Shaun Jusa/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma