Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping ampongeza Sheinbaum kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Mexico
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma salamu za pongezi kwa Claudia Sheinbaum Pardo siku ya Jumanne, akimpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Mexico. Kwenye salamu za pongezi, Rais Xi ameeleza kuwa Mexico ni nchi kubwa katika Amerika ya Kusini na ni nchi muhimu yenye soko linaloibukia na kwamba China na Mexico ni wenzi wa kimkakati wa pande zote.
Rais Xi amesema, Uhusiano wa China na Mexico umedumisha maendeleo mazuri, ukionesha ushirikiano wa kimkakati, wa kusaidiana na kunufaishana siku hadi siku, uhusiano huo upo katika kipindi muhimu cha kujenga kwenye mafanikio yaliyopita na kusonga mbele.
Rais Xi pia amesema, anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Mexico, na ningependa kuimarisha mawasiliano ya kimkakati na rais mteule Sheinbaum ili kuongoza uhusiano wa pande mbili uendelee kwenye ngazi mpya na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi zetu mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma