Lugha Nyingine
Rais Xi kuhudhuria hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 10 wa mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na nchi za Kiarabu
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China atahudhuria hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 10 wa mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na nchi za Kiarabu na kutoa hotuba kuu, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Hua Chunying ametangaza siku ya Jumapili.
“Kama ilivyokubaliwa na China na upande wa Nchi za Kiarabu, mkutano huo utafanyika Mei 30 mjini Beijing. Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Waziri wa Mambo ya Nje wa China ataongoza mkutano huo pamoja na mwenyekiti wa upande wa nchi za kiarabu Mohamed Salem Ould Merzouk, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Mauritania. Na mawaziri wa mambo ya nje au wajumbe wa nchi za Kiarabu na katibu mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu watahudhuria mkutano huo," Hua amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma