Lugha Nyingine
Uwekezaji wa kuvunja rekodi waashiria?ukuaji wenye nguvu wa eneo la Magharibi ya China
Watu wakihudhuria hafla ya ufunguzi wa Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya Eneo la Magharibi ya China mjini Chongqing, kusini-magharibi mwa China, Mei 23, 2024. (Xinhua/Wang Quanchao)
CHONGQING - Rekodi ya juu ya miradi mikubwa 196 imetiwa saini kwenye Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya Eneo la Magharibi ya China, ambayo yamefunguliwa Alhamisi mjini Chongqing, kusini-magharibi mwa China, huku miradi kutoka nchi na maeneo 12 ikipangwa kuanzishwa katika eneo la magharibi nchini China.
Maonyesho hayo ya siku nne ni maonyesho ya kwanza ya aina yake baada ya kongamano lililofanyika tarehe 23 Aprili kuhusu kuhimiza maendeleo ya eneo la magharibi nchini China katika zama mpya. Yanaashiria nia thabiti ya China ya kupanua ufunguaji mlango na ushirikiano.
Maonyesho hayo yanashirikisha kampuni zaidi ya 1,700 kutoka nchi na kanda 40, ikiwa ni pamoja na Walmart na Continental AG, na kutoka maeneo 27 ya ngazi ya mikoa nchini China. Washiriki pia ni pamoja na viongozi na wataalam kutoka mashirikisho ya wafanyabiashara wa kimataifa na wa ndani ya China.
Eneo la magharibi la China, ambalo linachukua karibu theluthi mbili ya ukubwa wa eneo la ardhi la nchi hiyo, lina nguvu kubwa za kifursa katika gharama za mambo ya uzalishaji na nguvu za maendeleo. Mwaka 2023, thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji nje bidhaa ya eneo hilo ilifikia yuan trilioni 3.7 (kama dola za kimarekani bilioni 511), ikiwa ni ongezeko la asilimia 37 ikilinganishwa na Mwaka 2019.
Miradi hiyo 12 ya uwekezaji wa kigeni yenye thamani ya jumla ya yuan zaidi ya bilioni 26.7 inahusiana na sekta mbalimbali, zikiwemo za magari ya teknolojia za kisasa yanayotumia nishati mpya, vifaa vya kisasa na uzalishaji bidhaa kwa kutumia teknolojia za kisasa, na mambo ya kisasa ya fedha. Nchi na maeneo kama vile Russia, Hispania na Japan zinashiriki.
Zhai Kun, profesa katika chuo cha Taaluma za Mambo ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Peking, amesema, "Kwa kuendana na mwelekeo wa kihistoria wa utandawazi wa uchumi, China inashikiria kithabiti katika kupanua ufunguaji mlango, kunufaika fursa za maendeleo zinazoletwa na ukuaji wa uchumi, na kuendelea kuongeza nguvu katika uchumi unaotetereka na wenye changamoto wa kimataifa."
Watu wakitembelea Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya Eneo la Magharibi ya China mjini Chongqing, kusini-magharibi mwa China, Mei 23, 2024. (Xinhua/Wang Quanchao)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma