Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping aongoza kongamano, ahimiza mageuzi zaidi ili kuendeleza ujenzi wa Mambo ya Kisasa wa China
Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akiongoza kongamano lililohudhuriwa na wajumbe wa sekta ya viwanda na kampuni na wanataaluma na kutoa hotuba muhimu mjini Jinan, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Mei 23. 2024. (Xinhua/Ju Peng)
JINAN - Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) siku ya Alhamisi wakati akiongoza kongamano mjini Jinan, Mkoa wa Shandong, lililohudhuriwa na wajumbe wa sekta za viwanda na kampuni na wanataaluma amesisitiza kuendeleza zaidi kwa kina mageuzi katika sekta zote kwa juhudi kubwa zaidi za kuhimiza kazi kuu ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.
Rais Xi amesema, "Mageuzi ndiyo msukumo kwa maendeleo," ili mageuzi yaendelee kwa kina zaidi katika pande zote, juhudi zinapaswa kuelekezwa kwenye malengo makuu ya kukamilisha na kuendeleza mfumo wa kijamaa wenye umaalum wa China, na kuufanya mfumo na uwezo wa utawala wa nchi kuwa wa kisasa.
Ameongeza kuwa, China inapaswa kuondoa madosari na upungufu katika fikra, mawazo, mifumo na utaratibu vinavyozuia kuhimiza maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China, na kuongeza maradufu juhudi zake za kuondoa vizuizi vya kimfumo na kitaratibu pamoja na migongano ya kimuundo.
Ziara hiyo ya Rais Xi mkoani Shandong ni ukaguzi wake wa kwanza kuufanya mikoani tangu Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC kufanya mkutano Aprili 30.
Iliamuliwa kwenye mkutano huo kuwa mkutano wa tatu wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC kitafanyika mjini Beijing mwezi Julai, na kwamba kikao hicho kitatathmini hasa masuala yanayohusu kuimarisha mageuzi ya pande zote na kuendeleza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.
Wajumbe tisa wa viwanda vya kiserikali, viwanda vya kiraia na vya ubia na nje walizungumza kwenye kongamano hilo kutoa maoni na mapendekezo juu ya kuimarisha mageuzi katika sekta zote, ambayo yanahusu masuala ya kuendeleza uwekezaji wa kuanzisha shughuli, uboreshaji wa viwanda vya jadi, kukamilisha usimamizi wa makampuni binafsi na kuboresha mazingira ya biashara kwa kampuni za kigeni.
Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akiongoza kongamano lililohudhuriwa na wajumbe wa sekta za viwanda na kampuni na wanataaluma na kutoa hotuba muhimu mjini Jinan, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Mei 23. 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)
Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akiongoza kongamano lililohudhuriwa na wajumbe wa sekta za viwanda na kampuni na wanataaluma na kutoa hotuba muhimu mjini Jinan, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Mei 23. 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)
Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akiwasiliana na wajumbe wa sekta za viwanda na kampuni na wanataaluma waliohudhuria kongamano mjini Jinan, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Mei 23. 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma