Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa pongezi kwa Rais mpya wa Vietnam
BEIJING – Siku ya Jumatano, Rais wa China Xi Jinping amempongeza To Lam kwa kushika wadhifa wa Rais wa Jamhuri ya Kijamaa ya Vietnam, ambapo kwenye pongezi zake hizo ameeleza kuwa China na Vietnam ni nchi majirani rafiki za kijamaa zinazounganishwa na milima na mito.
Rais Xi pia amesema kuwa kwenye ziara yake nchini Vietnam mwaka jana, yeye na Nguyen Phu Trong, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam, kwa pamoja walitangaza ujenzi wa jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja ambayo inabeba umuhimu wa kimkakati, ikifungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya Vyama na nchi hizo mbili.
Kiongozi huyo wa China amesema anafurahi kuona idara na sehemu mbalimbali za nchi hizo mbili zinaongeza juhudi za kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja, na kupata maendeleo.
Rais huyo wa China amesema anajali sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Vietnam, na angependa kufanya juhudi pamoja na komredi rais huyo katika kudumisha mawasiliano ya kimkakati, na kuelekeza ujenzi wa jumuiya ya China na Vietnam yenye mustakabali wa pamoja uendelee kwa kina na kupata maendeleo halisi, na kutoa manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma