Lugha Nyingine
Rais?Xi Jinping atoa salamu za pongezi kwa rais mteule wa Chad
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 22, 2024
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma ujumbe kwa Mahamat Idriss Deby Itno siku ya Jumatatu, akimpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Chad.
Rais Xi amesema, katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya China na Chad umedumisha kasi nzuri ya maendeleo, huku kuaminiana kwao kisiasa kukizidishwa kila siku, ushirikiano ukiendelea katika sekta mbalimbali, na ushirikiano katika mambo ya kimataifa unakuwa karibu zaidi.
Rais Xi amesema anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Chad na angependa kufanya juhudi pamoja na rais mteule huyo katika kuimarisha hali ya kuungana mkono na kuhimiza ushirikiano wa kirafiki, ili kunufaisha zaidi watu wa pande hizo mbili.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma