Lugha Nyingine
Bandari kubwa zaidi ya nchi kavu ya China yashughulikia treni za mizigo zaidi ya 1,700 za China-Ulaya
Kreni ikipakia makontena katika Stesheni ya Reli ya Manzhouli huko Manzhouli, Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China, Julai 1, 2020. (Xinhua/Yu Jia)
HARBIN - Bandari ya reli ya Manzhouli, ambayo ni bandari kubwa zaidi ya nchi kavu ya China, imeshughulikia safari 1,724 za treni za mizigo zinazotoa huduma kati ya China na Ulaya mwaka huu hadi kufikia siku ya Jumatano, ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.2 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, Shirika la Reli la China Tawi la Harbin limesema.
Bandari iliyo iliyo katika Mkoa Unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani wa China imeshughulikia makotena 184,000 (ya futi 20) ya bidhaa tangu Januari 1, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.8 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana.
Treni za mizigo za China na Ulaya zinazopitia bandari hiyo zinaunganisha miji 60 ya China na nchi 13 za nje, zikiwemo Russia, Poland na Ujerumani, zikisafirisha bidhaa kama vile bidhaa za umeme, mboga na magari.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma