Lugha Nyingine
China yaharakisha?mageuzi?ya kidijitali katika sekta ya uzalishaji viwandani
Picha ya kumbukumbu ikionyesha Kituo cha Pili cha Uzalishaji wa Hali ya Juu cha NIO huko Hefei, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China. (Xinhua)
BEIJING - China imeanza kufanya juhudi kubwa zaidi katika mageuzi ya kidijitali ya sekta ya uzalishaji viwandani ili kukuza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora na kuimarisha kasi ya ukuaji wa uchumi wake.
Baraza la Serikali la China kwenye mkutano wake wa utendaji hivi karibuni lilipitisha mpango wa utekelezaji unaolenga kuendeleza mambo ya kidijitali katika sekta ya uzalishaji viwandani. Mpango huo unajumuisha hatua za kukidhi mahitaji ya uzalishaji viwandani katika hali mbalimbali, kuharakisha maendeleo ya kiteknolojia, na kuimarisha juhudi za uungaji mkono kuanzia kuweka viwango hadi kujenga majukwaa ya huduma.
Mageuzi ya kidijitali ni ufunguo wa kuendeleza maendeleo mapya ya viwanda na ujenzi wa mfumo wa kisasa wa viwanda, kwa mujibu wa mkutano huo.
Kwa vile viwanda vya China vimeingia kwenye hatua muhimu katika kuhamia kwao kidijitali, sera mpya za serikali zitatoa mwongozo kwao ili kuharakisha kasi yao ya kidijitali na kuwezesha matumizi na uvumbuzi wa kiteknolojia, kwa mujibu wa wataalam.
Zhu Minghao, profesa katika Chuo Kikuu cha mawasiliano cha Beijing, amesema kuwa sekta ya uzalishaji viwandani ya kidijitali ni muhimu kwa maendeleo ya nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora, kwani mafungamano ya kina ya uchumi wa kidijitali na uchumi halisi yataunda mtindo mpya wa biashara, miundo mipya na huduma mpya.
Kwa miaka mitatu mfululizo, China imezindua miradi ya majaribio ya viwanda vya teknolojia za kisasa, kujenga viwanda 421 vya kielelezo vya ngazi ya kitaifa pamoja na karakana za kidijitali na viwanda vya teknolojia za kisasa zaidi ya 10,000 vya ngazi ya mikoa.
Teknolojia kama vile akili bandia na dijitali pacha zimetumika katika viwanda vya kielelezo zaidi ya asilimia 90. Teknolojia ya 5G imeendelezwa kwa kiwango kikubwa katika ukaguzi wa ubora, uzalishaji wa madini na sekta nyingine. Mtandao wa intaneti viwandani sasa unatumika katika sekta zote kuu, na mifano ya matumizi zaidi ya 200 imeanzishwa.
Kwenye ziara ya ukaguzi wiki iliyopita katika Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, ambao ni kituo kikuu cha viwanda cha China, Naibu Waziri Mkuu wa China Zhang Guoqing alisisitiza haja ya kuunga mkono kampuni ndogo na za kati kufanyamageuzi ya kidijitali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma