Lugha Nyingine
Mkoa wa Qinghai wa China wazindua mradi wa umeme wa 750-kV unaounganisha nishati mbadala kwenye gridi
Picha iliyopigwa Mei 7, 2024 ikionesha mradi wa kupitisha na kupoza umeme wa 750-kV katika Wilaya ya Gonghe, Mkoa wa Qinghai wa China. (Picha na Dong Qingfang/Xinhua)
Mradi wa kupitisha na kupoza umeme wa 750-kV umekamilika na kuanza kufanya kazi katika Mkoa wa Qinghai, Kaskazini Magharibi mwa China, imesema Kampuni ya Nishati ya Umeme wa Gridi ya Taifa ya China tawi la Qinghai.
Mradi huo ulio kwenye mwinuko wa mita 3,175 juu ya usawa wa bahari katika Wilaya ya Gonghe ya mkoa huo utasaidia kuunganisha umeme unaozalishwa na miradi ya nishati mbadala ya mkoa huo, ikiwemo miradi ya kuzalisha umeme kwa jua na upepo kwenye gridi ya taifa ya China.
Mradi huo unatarajiwa kuongeza uzalishaji wa nishati mbadala wa kila mwaka kwa zaidi ya kilowati-saa bilioni 9, ambayo ni sawa na kupunguza matumizi ya kaboni sanifu kwa karibu tani milioni 3.12 na kupunguza utoaji wa gesi ya kaboni kwa tani milioni 8.64.
Mkoa wa Qinghai ni chanzo cha mito mikuu ya China ya Mto Yangtze, Mto Manjano na Mto Lancang, na unajulikana kwa rasilimali zake nyingi za nishati ya maji, jua na upepo. Kwa jumla uwezo wa nishati mbadala uliofungwa mkoani humo ulifikia kilowati milioni 51.07 mwaka 2023.
Wafanyakazi wa kampuni ya Gridi ya Taifa ya China tawi la Qinghai wakifanya kazi kwenye mradi wa umeme wa 750-kV katika Wilaya ya Gonghe, Mkoa wa Qinghai, Kaskazini Magharibi mwa China, Aprili 23, 2024. (Picha na Wang Xiaogang/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma