Lugha Nyingine
China kuendelea kupanua ufunguaji mlango, kuchangia gawio la maendeleo: Makamu Rais wa China
Makamu Rais wa China Han Zheng akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kilele 2024 wa Uhimizaji wa Biashara na Uwekezaji wa Dunia nzima mjini Beijing, China, Mei 13, 2024. (Xinhua/Wang Ye)
BEIJING - China itaendelea kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu na kuchangia gawio lake la maendeleo na pande zote, Makamu Rais wa China Han Zheng amesema siku ya Jumatatu wakati akihutubia ufunguzi wa Mkutano wa Kilele 2024 wa uhimizaji wa Biashara na Uwekezaji wa Dunia nzima mjini Beijing.
Ni kwa kuhimiza biashara na uwekezaji huria bila kuyumba, na kulinda kihalisi uhimilivu na utulivu wa minyororo ya utoaji wa bidhaa wa viwanda ya dunia nzima, ndipo ushirikiano unaweza kuimarishwa na kunufaishana kuweza kupanuliwa, Han amesema.
Ametoa wito wa juhudi za kutumia fursa ya duru mpya ya mapinduzi ya kiteknolojia na kiviwanda, kuimarisha uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, na kuendeleza vichocheo vipya vya ukuaji wa uchumi.
“China ikiwa ni nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi wake duniani, mchango wake kwa ukuaji wa uchumi wa dunia umedumisha karibu asilimia 30 kwa miaka mingi,” Han amesema, huku akiongeza kuwa China ingependa kunufaika pamoja na dunia fursa za China za maendeleo endelevu, na inakaribisha kampuni za nchi mbalimbali duniani kuendelea kuwekeza nchini China ili kuendeleza shughuli zao na kupata maendeleo yao nchini China.
Mkutano huo wa tatu umeandaliwa na Shirika la China la Uhimiza wa Biashara ya Kimataifa.
Watu zaidi ya 750 kutoka mashirika ya kimataifa, mashirikisho ya wafanyabiashara wa nje, mashirika ya uhimizaji wa biashara ya dunia nzima, wajumbe wa kampuni za China wameshiriki kwenye mkutano huo.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma