Lugha Nyingine
Sekta?ya uzalishaji?wa?magari ya China yarekodi ukuaji thabiti katika robo ya kwanza ya Mwaka 2024
Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye mstari wa kuunganisha sehemu za magari wa kiwanda cha kampuni ya Voyah, ambayo ni chapa ya magari ya kifahari yanayotumia umeme ya China, huko Wuhan, Mkoa wa Hubei, katikati ya China, Aprili 1, 2024. (Xinhua/Xiao Yijiu)
BEIJING – Sekta ya uzalishaji wa magari ya China imerekodi ongezeko kubwa katika robo ya kwanza (Q1) ya mwaka huu wa 2024, takwimu mpya kutoka Shirikisho la sekta ya Magari la China zinaonesha.
Katika kipindi hicho, thamani iliyoongezwa ya sekta hiyo iliongezeka kwa asilimia 9.7 mwaka hadi mwaka, ambayo ni asilimia 3 zaidi ya ile ya sekta ya viwanda kwa ujumla ya China, kwa mujibu wa shirikisho hilo.
Mapato ya jumla ya sekta hiyo yalifikia yuan trilioni 2.25 (kama dola za Kimarekani bilioni 316.85), ikiwa ni ongezeko la asilimia 6.2 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana.
Faida ya jumla ya kampuni za sekta hiyo iliongezeka kwa asilimia 32 kwa mwaka hadi yuan bilioni 103.95, takwimu hizo zimesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma