Lugha Nyingine
Xi Jinping ashiriki kwenye karamu ya kumkaribisha iliyoandaliwa na rais wa Serbia
Picha hii ikionesha Xi akitoa hotuba fupi ya shukrani kwenye karamu. (Picha na Pang Xilei/Xinhua)
Mchana wa tarehe 8, Mei, rais wa China Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan walishiriki kwenye karamu ya makaribisho iliyoandaliwa na rais wa Serbia Aleksandar Vucic na mkewe kwenye Jumba la Serbia huko Belgrade, Serbia.
Chini ya hali ambayo makofi ya furaha zaidi yalipigwa ukumbini humo, rais Xi alitoa hotuba fupi ya shukrani.
Xi alisema, watu wa China wana urafiki maalumu kwa Serbia, filamu iitwayo “Daraja” ya Yugoslavia ilioneshwa zaidi nchini China na Wachina wengi wanapenda sana wimbo wa “Kwa heri Bella” kwenye filamu hiyo. Katika miaka ya hivi karibuni, China na Serbia zimejenga pamoja kwa nguvu kubwa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na zimepata mafanikio makubwa. Juhudi hizo zimekuwa uzoefu halisi wa ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma