Lugha Nyingine
Ofisa wa Zimbabwe aipongeza mchango wa Huawei katika kuhimiza maendeleo ya kidigitali nchini Zimbabwe
(CRI Online) Mei 08, 2024
Katibu mkuu wa wizara ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari, Posta na Huduma za Vifurushi wa Zimbabwe Bw. Beaullar Chirume, ameipongeza kampuni ya Huawei ya China kwa juhudi zake katika kuendeleza mambo ya kidigitali nchini Zimbabwe.
Kwenye mahojiano yaliyofanyika mjini Harare kwenye baraza la Huawei la Zimbabwe 2024, Bw. Chirume aliangazia mchango wa Huawei katika kuweka misingi ya miundombinu ya TEHAMA ya Zimbabwe kupitia ushirikiano na China.
Amesema katika miaka 25 iliyopita, Zimbabwe imeshuhudia mchango wa kampuni ya Huawei katika dira ya nchi hiyo kuendeleza uchumi wa kidigitali. Mbali na kuendeleza miundombinu, Bw. Chirume pia ameangazia juhudi za Huawei katika kusaidia kuwaandaa vipaji vya TEHAMA nchini Zimbabwe.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma