Lugha Nyingine
Wimbi la Safari ya likizo ya Siku ya Wafanyakazi nchini China laonesha uhai wa uchumi
Tarehe 4, Mei, 2024, watu wakitembelea kituo cha manunuzi cha Chongqing, China. (Picha na Huang Wei/Xinhua)
Katika likizo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ya China iliyoanzia tarehe Mosi hadi 5 mwezi huu, Wachina wengi walisafiri katika sehemu mbalimbali nchini, hali ambayo imeonesha uhai na uhimilivu wa uchumi wa China.
Mji wa Chongqing wa Kusini Magharibi mwa China unaojulikana kwa mtindo wake wa maisha ya burudani na chakula cha kipekee cha pilipilihoho siku zote ukiwa umekuwa moja kati ya vivutio vya utalii vinavyopendwa zaidi. Takwimu kutoka serikali ya mji huo imeonesha kuwa, katika siku tatu za kwanza za likizo hiyo, mapato ya utalii ya mji mzima yamefikia Yuan bilioni 4.28 (sawa na Dola milioni 591 za Marekani), yakiongezeka kwa asilimia 17.5 kwa kulinganishwa na yale ya kipindi kama hicho mwaka jana.
Tarehe Mosi , Mei, 2024, watalii wakicheza kwenye Kijiji cha Zhuquan, Wilaya ya Yinan ya Mji wa Linyi wa Mkoa wa Shandong, China. (Picha na Wang Yanbing/Xinhua)
Wakati wa likizo hiyo, kutokana na kuboreshwa kwa miundombinu na kuongezeka kwa uwezo wa kuwapokea watalii, masoko ya utalii ya ngazi ya chini yamevutia watalii wengi zaidi.
Ikikadiriwa na Trip.com, katika wakati wa likizo hiyo, oda za hoteli katika masoko ya ngazi ya wilaya zimeongezeka kwa asilimia 68. Takwimu pia zinaonesha kuwa safari za utalii katika vijiji zimeongezeka kwa asilimia 42 zikilinganishwa na zile za kipindi kama hicho mwaka jana.
Shirika la Reli la China limekadiria kuwa, katika kipindi cha kilele cha safari cha Siku ya Wafanyakazi kuanzia tarehe 29, Aprili hadi tarehe 6, Mei, mtandao wa reli wa China umeshughulikia safari milioni 144 za abiria.
Picha hii iliyopigwa tarehe 1, Mei, 2024 ikionesha abiria ndani ya ukumbi wa kusubiria treni katika Stesheni ya Treni ya Shanghai Hongqiao. (Picha na Wang Xiang/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma