Lugha Nyingine
Wanasayansi wakuza kwa haraka mpunga kando ya jangwa
Watafiti wakikuza miche ya mpunga kwa kutumia kiowevu chenye virutubisho katika kibanda cha kilimo kilichopo kwenye ardhi ya Hotan, Eneo linalojiendesha la Kabila la Wauygur la Xinjiang, China. (Picha/ChinaDaily)
Kutokana na teknolojia ya kilimo kisichohitaji udongo, vifaa vya utoaji mwanga na teknolojia nyingine, hivi sasa muda wa ukuaji wa mpunga unaopandwa kando ya Jangwa la Taklimakan la Xinjiang umepungua kwa dhahiri.
Wanasayansi wa Taasisi ya Sayansi ya Kilimo ya China hivi karibuni wametangaza kuwa, walifanya majaribio ya kupanda mpunga wa aina ya kawaida katika kibanda cha kilimo kilichojengwa kwenye ardhi kubwa ya Hotan, Kusini mwa Xinjiang, ambapo mpunga huo ulipevuka baada ya siku 60 tu, muda huo ambao haufikii nusu ya muda wa kawaida.
Ndani ya kibanda, mpunga unapandwa kwenye kiowevu chenye virutubisho katika rafu, hali ambayo inasaidia kutumia nafasi ndogo zaidi, na vifaa vya kutoa mwanga pia vinatumiwa kwa ajili ya ukuaji wa mpunga siku zote.
Mwanasayansi mkuu wa Idara ya utafiti wa kilimo ya miji ya Taasisi ya Killimo ya China, ambaye pia ni kiongozi wa mradi huo Yang Qichang alisema kuwa, “Hotan ina jangwa kubwa na rasilimali nzuri ya mwanga na joto, kwa hivyo ni sehemu bora ya kufanya utafiti wa kilimo kwa kutumia ardhi iliyotelekezwa."
Wang Sen, mtafiti wa taasisi hiyo anayeshiriki kwenye mradi huo alisema, wenzake wanajaribu kutumia teknolojia hiyo hiyo kuharakisha kuotesha mimea mingine kwenye jangwa, ikiwemo viazi, mahindi, ngano, mipamba n.k.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma