Lugha Nyingine
Mfumo wa droni za kibiashara uliotengenezwa na China uko tayari kwa urukaji wa mara ya kwanza wa droni zake
Picha hii ya data ikionesha droni ya HH-100 ikifanyiwa majaribio kwenye uwanja wa ndege wa Beichuan Yongchang wa Mkoa wa Sichuan, China. (Picha iliotolewa na Kampuni ya Kundi la AVIC na kuchapishwa na Xinhua)
Habari kutoka Kampuni ya Kundi la Viwanda vya Usafiri wa Anga la China (AVIC) zinasema, mfumo mpya wa droni za kibiashara (UAS) uliotengenezwa na China yenyewe umeingia kipindi chake cha urukaji wa kwanza kwa droni.
Kampuni ya viwanda vya kuongoza vya uundaji wa ndege ya China ilisema, droni ya HH-100 yenye uwezo mbalimbali hivi karibuni imekamilisha majaribio yake ya mwisho ya kuteleza kwa kasi kiotomatiki.
Kampuni hiyo ilisema, droni ya HH-100 ilipofanyiwa majaribio ilionekana urukaji wake tulivu, na uendeshaji wake wa kudhibiti hali ya kuteleza kiotomatiki ulifanyika vizuri. Sasa droni hiyo imeingia kwenye kipindi chake cha urukaji wa kwanza.
Mfumo wa Droni ya HH-100 ulitengenezwa kwa kujitegemea na kampuni ya ndege za kibiashara za AVIC XAC mkoani Shaanxi, kaskazini-magharibi mwa China. Mfumo huo unaundwa na sehemu kubwa mbili, droni na kituo cha kuziongoza na kuzidhibiti kwenye ardhi.
Droni hiyo ya kibiashara ina ubora wake wa gharama ya chini, na wa kubeba uzito mkubwa unaoweza kufikia kilo 700. Droni inaweza kuruka kwa kilomita 520 kwa kubeba uzito huo.
Kampuni ya AVIC ilisema, droni ya HH-100 inaweza kufanya kazi za usambazaji vitu, uzimamoto katika misitu na mbuga, ufuatiliaji na udhibiti wa maafa ya moto, na kusafirisha vifaa vya kuokoa maafa.
Picha hii ya data ikionesha droni ya HH-100 ikifanyiwa majaribio kwenye uwanja wa ndege wa Beichuan Yongchang cha Mkoa wa Sichuan, China. (Picha iliotolewa na Shirika la AVIC na kuchapishwa na Xinhua)
Watu watoa heshima kwa marehemu kabla ya siku ya Qingming katika Mji wa Beijing, China
Msanii wa Ethiopia abuni sanaa kutokana na ufunuo wa kitabu maarufu cha China “Yi Jing”
Treni yaendeshwa katikati ya maua karibu na sehemu ya Juyongguan ya Ukuta Mkuu wa Beijing
Sherehe za kuashiria kuanza kwa kilimo cha majira ya mchipuko zafanyika Mkoa wa Xizang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma