Lugha Nyingine
China yashuhudia watalii karibu milioni 119 wa ndani wakati wa likizo ya Qingming
Picha ikionesha watalii wakitembelea eneo la kivutio la Beiwudang mjini Shizuishan, Eneo linalojiendesha la Kabila la Wahui la Ningxia la Kasikazini Magharibi mwa China Aprili 5, 2024. (Xinhua/Feng Kaihua)
Takwimu kutoka Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China zimeonesha kuwa, katika likizo ya siku tatu wakati wa Siku ya Qingming iliyoishia Jumamosi wiki hii, watalii wa ndani ya China walifikia karibu milioni 119, idadi ambayo imeongezeka kwa asilimia 11.5 ikilinganishwa na kipindi hicho mwaka 2019.
Siku ya Qingming ni siku muhimu kwa Wachina kusafisha makaburi ya jamaa zao na kutambika mababu. Watu wengi pia wanafanya mapumziko au kusafiri wakati wa likizo hiyo ya siku tatu.
Katika likizo ya Siku ya Qingming, mapato ya jumla ya shughuli za utalii wa ndani ya China yalifikia Yuan bilioni 53.95 (takriban Dola za Marekani bilioni 7.6), ambayo imeongezeka kwa asilimia 12.7 ikilinganishwa na mwaka 2019.
Kuendesha magari wenyewe, kupanda baiskeli na kusafiri kwa kutembea kwa miguu zilikuwa njia za kupendwa zaidi za usafiri wa watu wakati wa likizo hiyo, huku safari ya masafa mafupi na safari ya sehemu wanazokaa zikipendelewa.
Katika wakati wa Siku ya Qingming, watalii kutoka nchi za nje waliosafiri nchini China walifikia milioni 1.04, na watalii wa China waliosafiri nchi nyingine walifikia laki 9.92, idadi ambayo ilikaribia ile ya mwaka 2019. Japan, Thailand na Korea Kusini zilikuwa mahali pa kupendwa zaidi kwa wasafiri wa China.
Watu watoa heshima kwa marehemu kabla ya siku ya Qingming katika Mji wa Beijing, China
Msanii wa Ethiopia abuni sanaa kutokana na ufunuo wa kitabu maarufu cha China “Yi Jing”
Treni yaendeshwa katikati ya maua karibu na sehemu ya Juyongguan ya Ukuta Mkuu wa Beijing
Sherehe za kuashiria kuanza kwa kilimo cha majira ya mchipuko zafanyika Mkoa wa Xizang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma