Lugha Nyingine
Shughuli za viwandani za China zafufuka mwezi Machi
Wafanyakazi wakiunganisha sehemu za mashine ya kupandia mbegu shambani katika karakana ya kampuni ya utengenezaji wa mashine za kilimo huko Jiamusi, Mkoa wa Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China, Machi 13, 2024. (Xinhua/Wang Jianwei)
BEIJING - Shughuli za viwandani nchini China zimepanuka mwezi Machi baada ya kudorora kwa miezi mitano mfululizo huku kampuni zikiripoti ufufukaji wa uzalishaji na mahitaji wa bidhaa na kuonyesha matumaini katika mtazamo wa shughuli zao.
Fahirisi ya wasimamizi wa ununuzi (PMI) kwa sekta ya viwanda nchini China ilikuwa 50.8 mwezi Machi, ikirejea kwa kuimarika kwenye eneo la upanuzi kutoka 49.1 mwezi Februari, Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) imesema Jumapili.
Fahirisi hiyo ikiwa zaidi ya 50 inaonyesha upanuzi, wakati ikiwa chini ya 50 inaonyesha kudorora.
Zhang Liqun, mchambuzi maalum wa Shirikisho la Usambazaji na Ununuzi Bidhaa la China, amesema kupanda juu kwa PMI mwezi Machi kunaonyesha athari za sababu za msimu na kasi ya ufufukaji wa ujumla kwa uchumi. Pia ameelezea kuwa sera nyingi zinazolenga kuleta utulivu wa ukuaji wa uchumi na kuongeza imani ya soko mwaka huu zinaanza kutekelezwa hatua kwa hatua.
Miongoni mwa sekta 21 zilizofanyiwa utafiti, 15 zilikuwa katika eneo la upanuzi mwezi Machi, ikiwa ni ongezeko la sekta 10 kutoka mwezi uliopita, wakati ambapo kampuni zinaharakisha uzalishaji baada ya likizo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.
Fahirisi ndogo ya uzalishaji katika sekta ya viwanda ilipanda kutoka 49.8 hadi 52.2 mwezi Machi, wakati fahirisi ndogo ya kupima idadi ya oda mpya iliongezeka kutoka 49 hadi 53, ikionyesha nguvu kubwa ya ufufukaji katika uzalishaji na mahitaji ya bidhaa.
Ongezeko la uuzaji na uagizaji wa bidhaa lilikuwa ongezeko lingine la sekta ya viwanda. Viwanda vya kemikali, magari na vifaa vya mawasiliano ya habari viliripoti kuboreka kwa biashara za nje ikilinganishwa na mwezi mmoja uliopita. Viwanda vya ukubwa tofauti vyote vimekuwa na hali ya kuboreshwa katika uzalishaji na uendeshaji mwezi huu. PMI ya viwanda vidogo ikirudi juu ya mstari wa faida na kustawi kwa mara ya kwanza katika miezi 12, wakati PMI kwa viwanda vikubwa imepanda hadi 51.1 kutoka 50.4.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma