Lugha Nyingine
China yawaandaa mafundi wa kizazi kipya na elimu ya ufundi wa kazi yastawi zaidi
Katika miaka ya hivi karibuni, China ikiwa imepanua elimu ya ufundi wa kazi kutokana na mahitaji ya viwandani. Kwa kupitia hatua mbalimbali, elimu ya ufundi wa kazi ya China inaelekea ushirikiano wa kimataifa.
Kuwaandaa watu wenye sifa bora ya ujuzi wa kazi
Karakana ya Luban imeonesha ushirikiano wa kunufaishana wa kimataifa katika elimu ya ufundi wa kazi. Karakana hiyo inayoitwa kwa jina la fundi maarufu wa China wa zama za kale inatoa mafunzo ya ufundi wa kazi katika nchi mbalimbali, zikiwemo Thailand, India, Indonesia n.k.
Takwimu zimeonesha kuwa, tangu pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” lilipotolewa miaka 10 iliyopita, Vyuo vya Ufundi wa Kazi zaidi ya 400 vya China vimeshirikiana na mashirika ya elimu ya nchi nyingine katika kutoa mafunzo, na Karakana ya Luban imeanzishwa katika nchi zaidi ya 20.
Picha iliyopigwa Februari 15, 2024 ikionesha muonekano wa karakana ya Luban katika Kituo cha Mafunzo ya Teknolojia na Ufundi wa Kazi cha Ethiopia mjini Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Li Yahui)
Na miradi mingi ya elimu ya ufundi wa kazi ya China imeingia nchi za ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, ili kuelimisha mafundi wa kazi wenye sifa bora.
Mnamo mwaka 2017, Reli ya Mombasa-Nairobi (SGR) iliyojengwa chini ya ushirikiano wa Kampuni ya Barabara na Daraja ya China (CRBC) na serikali ya Kenya ilizinduliwa rasmi. Vyuo viwili vya elimu ya ufundi wa kazi kutoka mkoa wa Liaoning wa China vimetuma walimu kwenda katika Kenya, ambao wamewaandaa mafundi zaidi ya 300 wenye sifa bora kwa ajili ya reli hiyo ya Kenya.
Kwa sasa, China imekuwa na mfumo mkubwa zaidi wa elimu ya ufundi wa kazi duniani.
Miradi ya Ng’ambo
Ili kuhudumia kampuni za China zinazoendeleza shughuli zao katika nchi za nje, vyuo 18 vya elimu ya ufundi wa kazi vya Mkoa wa Guangdong, China vimeanzisha miradi 39 ya elimu ya ufundi wa kazi katika nchi nyingine.
Wanafunzi wakishiriki kwenye mradi wa ufundi wa kazi unaoendeshwa na kampuni ya magari ya BMW Brilliance (BBA) huko Shenyang, Mkoa wa Liaoning wa China Machi 20, 2024. (Xinhua/Pan Yulong)
Licha ya hayo, China inaalika kampuni za kimataifa kuchangia maendeleo ya elimu ya ufundi wa kazi ya China.
Kuanzia mwaka 2013, kampuni ya magari ya BMW Brilliance (BBA) iliyoko Shenyang, Mkoa wa Liaoning wa China ikiwa imeendesha miradi ya mafunzo ya ufundi wa kazi. Kwa sasa vyuo viwili vya ufundi wa kazi vinashirikiana na BBA katika ujenzi wa miradi. Kila mwaka kampuni hiyo inachagua wanafunzi kutoka vyuo vya ufundi wa kazi na vituo vya mafunzo na kuwapeleka kufanya mazoezi ya kazi, na wanafunzi hao wakipita mtihani watapata nafasi ya ajira.
“Kwa sababu ya mradi huo, nilipata ajira mara moja baada ya kuhitimu,” alisema Sun Haoran, mtengenezaji kwenye mnyororo wa uzalishaji wa BBA mwenye umri wa miaka 22.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma