Lugha Nyingine
Marais wa China na Honduras wapongezana kwa kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili
Rais Xi Jinping wa China na Rais Xiomara Castro wa Honduras wamepeana salamu za pongezi za kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.
Katika salamu hizo, rais Xi ameisifu Honduras kwa kushikilia kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, na kusisitiza kuwa China inaweka mkazo mkubwa katika kukuza uhusiano na Honduras. Pia amesema anapenda kushirikiana na rais Castro kufanya juhudi za pamoja, kuimarisha kuungana mkono, na kupanua ushirikiano katika pande zote, ili kuandika kwa pamoja ukurasa mpya wa mustakabali bora kwa uhusiano kati ya pande hizo mbili.
Kwa upande wake rais Castro amesisitiza kuwa Honduras itafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, na kupenda kuimarisha uhusiano na China kwenye msingi wa kujitawala na kujiamulia, na kuheshimiana.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma