Lugha Nyingine
China yasema itapanua zaidi ufungua mlango wa kiwango cha juu kwa uwekezaji wa nje
Picha iliyopigwa Septemba 10, 2023 ikionesha mandhari ya eneo la Zhangjiang la Eneo la Majaribio la Biashara Huria la China (Shanghai). (Xinhua/Fang Zhe)
Wizara ya Biashara ya China tarehe 25 ilisema kuwa, China itapanua zaidi ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, ili kutoa fursa nyingi zaidi kwa wawekezaji wa kigeni kuendesha biashara yao kwa kina zaidi nchini China.
Naibu Waziri wa Biashara wa China Guo Tingting kwenye mkutano wa Jukwaa la Maendeleo la China 2024 alisema kuwa, kutokana na China kuondoa kwa mfululizo vizuizi vya kuingia soko la China la sekta ya utengenezaji wa bidhaa, ufungaji mlango utahimizwa katika sekta ya mawasiliano ya habari, matibabu na n.k., kwa hivyo utaleta fursa nyingi zaidi za kufanya biashara na kuwekeza kwa wawekezaji wa kigeni.
Guo alisema, China pia itachukua hatua za kuhimiza uwekezaji, na kuboresha zaidi huduma husika ili kuhakikisha kampuni za nchi za nje zinapata huduma sawa kama raia wa China.
“Tutaimarisha zaidi juhudi za kuhamasisha kufanya uvumbuzi, na kushiriki kwa hamasa kwenye ushirikiano wa minyororo ya viwanda ya uzalishaji na utoaji wa bidhaa duniani,” alisema Guo, akiongezea kuwa China itafanya juhudi kuendeleza teknolojia mpya, viwanda vipya na mitindo mipya ya biashara, kupanua biashara ya huduma na biashara ya kidijitali, ili kuhimiza maendeleo ya kampuni kwa kutegemea uvumbuzi.
Guo alisema, China itaendeleza kwa kina ushirikiano wa pande nyingi na wa pande mbili mbili, kusukuma Kundi la nchi 20 (G20), Shirika la Ushirikiano wa Uchumi la Asia Pasifiki (APEC), kundi la BRICS na mifumo mingine kupata matunda mengi zaidi halisi, ili utandawazi wa uchumi duniani unufaishe zaidi pande zote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma