Lugha Nyingine
Takwimu?za fedha za kigeni nchini China zaonyesha matarajio mazuri ya mali zinazotegemea Yuan
Picha hii iliyopigwa tarehe 10 Januari 2023 ikionyesha eneo la Lujiazui katika Eneo la Majaribio ya Biashara Huria la China mjini Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Fang Zhe)
BEIJING - Soko la mabadilishano ya fedha za kigeni la China limepata ufanisi mzuri mwezi wa Februari mwaka huu, likiwa na mtiririko thabiti zaidi wa mtaji unaovuka mpaka, ikionyesha ushawishi wa kudumu na matarajio yenye mustakabali mzuri ya mali zinazotegemea sarafu ya China, Yuan, kwa mujibu wa wachambuzi.
Takwimu kutoka Idara ya Usimamizi wa Mabadilishano ya Fedha za Kigeni zinaonesha kuwa, benki za biashara nchini China zimeshuhudia ziada ya malipo ya Yuan bilioni 12 (takriban dola za kimarekani bilioni 1.69) mwezi Februari.
Kwa kuhesabiwa na Yuan, manunuzi ya fedha za kigeni yaliyofanywa na benki yalifikia takriban yuan trilioni 1.09, wakati mauzo yalifikia Yuan trilioni 1.08.
Kuongezeka kwa nia ya kuwekeza nchini China
Uingiaji wa jumla wa fedha za kigeni ya biashara ya bidhaa na uwekezaji wa dhamana vyote vilibaki katika kiwango cha juu mwezi wa Februari, amesema Wang Chunying, naibu mkurugenzi na msemaji wa idara hiyo.
Uingiaji wa kila siku wa fedha za kuvuka mpaka yabiashara ya bidhaa, ukiacha athari za likizo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China na mambo mengine, uliongezeka kwa asilimia 3 mwaka hadi mwaka katika kipindi hicho, hali ambayo inaendelea kusisitiza misingi ya mtiririko wa mtaji wa kuvuka mpaka, Wang amesema.
Mvuto wa muda mrefu wa soko la China
Akiangazia siku zijazo, Wang amesema soko la mabadilishano ya fedha za kigeni la China litadumisha ufanisi thabiti, likiimarishwa na misingi thabiti ya uchumi wa nchi, sera thabiti za uungaji mkono na kukua kwa unyumbufu wa soko.
Ameelezea sababu kama vile juhudi za China katika kuimarisha udhibiti wa jumla ili kuhimiza kasi ya kuimarika kwa uchumi Mwaka 2024, kuendeleza kwa kasi ufunguaji mlango wa kitaasisi, na kuboresha mazingira ya biashara ili kuwezesha biashara, uwekezaji na utafutaji fedha wa kuvuka mipaka.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma