Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa wito wa juhudi madhubuti za kustawisha zaidi Eneo la Kati la China
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiongoza kongamano la kulihimiza eneo la kati la China listawi na kujitokeza katika zama mpya huko Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati ya China, Machi 20, 2024. (Xinhua/Ju Peng)
CHANGSHA - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) siku ya Jumatano wakati akiongoza kongamano la kuhimiza eneo la kati la China listawi na kujitokeza katika zama mpya, ameagiza kufanyika juhudi madhubuti za kuimarisha na kustawisha zaidi eneo la katikati ya China kwa kuanzia kwenye mwanzo wenye kiwango cha juu.
Katika hotuba yake, Rais Xi amesisitiza kuwa, eneo la kati ni kituo muhimu cha uzalishaji nafaka wa China, ni kituo cha nishati na malighafi, ni kituo cha utengenezaji wa vifaa vya kisasa na viwanda vya kutumia teknolojia ya hali ya juu, na ni kituo kamili cha mawasiliano na uchukuzi, eneo hilo lina hadhi yake isiyoweza kupuuzwa kote nchini.
Rais Xi ametoa wito wa kufanya ushirikiano katika kuhimiza maendeleo yenye sifa bora na kuandika ukurasa mpya wa kuimarisha na kustawisha eneo la kati la China katika kuhimiza mchakato wa ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.
Li Qiang, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Kisiasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Waziri Mkuu wa China, Cai Qi, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya CPC na Ding Xuexiang, mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu wa China, walihudhuria kongamano hilo.
Tangu kongamano la kuhimiza eneo hilo la kati listawi na kujitokeza lifanyike miaka mitano iliyopita, maendeleo ya eneo hilo yamefikia kiwango cha juu zaidi, Rais Xi amesema.
Rais Xi pia amesisitiza kuwa kulihimiza eneo la kati la China listawi na kujitokeza bado kunakabiliwa na matatizo na changamoto nyingi ambazo zinahitaji utafiti wenye kuleta hatua halisi ili kuzitatua.
Juhudi zaidi zinapaswa kufanywa kusukuma mbele uvumbuzi wa viwanda unaoongozwa na uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, na kuhimiza kikamilifu nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora, amesema.
Rais Xi ametoa wito wa kupanga mipango ya kuendeleza viwanda kwa kutupia macho siku za baadaye, na kuharakisha kuanzisha mfumo wa viwanda vya kisasa vinavyotegemea utengenezaji bidhaa wenye kutumia teknolojia za hali ya juu.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiongoza kongamano la kulihimiza eneo la kati la China listawi na kujitokeza katika zama mpya huko Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati ya China, Machi 20, 2024. (Xinhua/Wang Ye)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma