Lugha Nyingine
China yatilia mkazo mfumo wa mambo ya fedha?wa "orodha nyeupe" ili kuleta utulivu kwenye soko la mali isiyohamishika
Picha iliyopigwa Juni 24, 2023 ikionyesha eneo la kati la Mji wa Tianjin, Kaskazini mwa China. (Xinhua/Sun Fanyue)
BEIJING - China inatilia mkazo mfumo wake wa mambo ya fedha wa "orodha nyeupe" kwa miradi ya mali isiyohamishika katika juhudi za kuleta utulivu kwenye soko ambapo Chini ya mfumo huo ulioanza mwishoni mwa Januari, serikali za mitaa zinapendekeza miradi ya mali isiyohamishika inayostahiki kupata uungaji mkonokutoka kwa taasisi za kifedha.
Pia serikali za mitaa zinaratibu kwa pamoja na taasisi za kifedha ili kutimiza matakwa ya miradi hiyo.
Mfumo huo ni sehemu ya juhudi za China za kuleta utulivu katika sekta hiyo inayolemewa na matatizo ya madeni na kuongeza imani katika sekta hiyo inayochangia karibu asilimia 6 ya Pato la Taifa, kwa mujibu wa Idara Kuu ya Taifa ya Takwimu ya China.
Hadi kufikia mwisho wa Februari, yuan zaidi ya bilioni 200 (kama dola za Kimarekani bilioni 28.17) zilikuwa zimeidhinishwa chini ya mfumo huo ili kusaidia miradi takriban 6,000 ya mali isiyohamishika katika miji 276 kote nchini China, takwimu kutoka Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji na Vijijini ya China zinaonyesha.
Mfumo wa "orodha nyeupe" unasaidia kuhakikisha kukamilika kwa miradi bora ya mali isiyohamishika iliyopangwa na kujengwa na kampuni ambazo zinasumbuliwa na masuala ya madeni, ameisema Zhang Dawei, mchambuzi mkuu katika wakala wa mali isiyohamishika, Centaline Property.
Liu Shui, mtafiti wa taasisi ya utafiti wa mali isiyohamishika ya China Index, amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza matatizo ya kifedha wa kampuni zinazopanga na kujenga miradi na kuleta utulivu wa matarajio ya soko.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma